Na mwandishi Maalum, Mtwara
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Ndugu Christina Mndeme amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji kufika Newala kesho Jumatatu Septemba 20, 2021 katika mradi wa maji Makonde mkoaoni Mtwara ili kutoa sulu ya mradi huo ambao haujatoa maji kwa takribani wiki tatu sasa.
Mndeme ametoa maagizo hayo wakati akizungumza baada ya kutembelea kituo cha kupokea maji kutoka kwenye chanzo cha maji Mkunya na kujionea mashine zikiwa zimeharibika.
Naibu Katibu Mkuu alisema”Tukiri kuna uzembe umefanyika hapa katikati haiwezekani mashine tangu mwaka 1954 mpaka leo zinatumika”
Ndugu Mndeme amesema maji hayana mbadala na amesikitishwa sana kuona hakuna hatua zinazochukuliwa kwa haraka katika kutatua tatizo la maji wilayani hapo.
Naibu Katibu Mkuu ameshangazwa na kuona fedha kiasi cha bilioni 11 zimepelekwa na Serikali lakini mradi haujafanyiwa marekebisho mpaka sasa.
Naibu Katibu yupo kwenye ziara ya Katibu Mkuu wa CCM pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM yenye lengo la kukagua, kusimamia na kuhamasisha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2021.
Post a Comment