Featured

    Featured Posts

NAIBU SPIKA: WANAWAKE,TGGA TUSHIKAMANE KUMSAIDIA RAIS SAMIA TANZANIA ISONGE MBELE +video

Naibu Spika wa Baraya la Wawakilishi Zanzibar, Mgeni Hassan Juma akizindua kitabu cha muongozo wa Chama cha Tanzania Girl  Guides (TGGA) wakati wa kufunga Kambi ya Mafunzo Elekezi kwa  Viongozi wapya wa chama hicho katika Shule ya Sekondari ya Ufundi Moshi, mkoani Kilimanjaro. Mafunzo hayo ya siku 6 yalianza Septemba 12 na kumalizika Septemba 17,2021. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TGGA, Anna Maembe na Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi.


Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Spika Mgeni ametoa wito kwa Skauti wa Kike na wanawake kwa ujumla kushikamana kwa kuchapa kazi kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika harakati ya kuhakikisha Tanzania inapiga hatua za kimaendeleo.

Katika hafla hizo mgeni rasmi huzo aliwaapisha viongozi wapya zaidi ya 150 kutoka mikoa 20 ya Tanzania Bara na Visiwani.






Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mgeni Hassan Juma ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini TGGA,  akihutubia wakati wa kufunga kambi hiyo. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA
 

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza/ kuona  kupitia clip hii ya video  ujue yalizojiri katika hafla hiyo ya kufunga kambi.....

Imeandaliwa na Richard Mwaikenda 
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 
0754264203
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana