Dar es Salaam, Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Septemba 23, 2021 anatarajiaa kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) katika Mkutano wa 76 wa Umoja Utakaofanyika mjini New York nchini Marekani.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu jijini Dar es Salaam imesema Rais Samia anatarajiwa kuondoka nchini leo Jumamosi Septemba 18, kwenda New York Marekani kwenda kuhudhuria Mkutano huo.
Pamoja na Mkutano huo, Rais Samia pia atahudhuria mikutano ya kilele ya kujadili masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs)
Aidha, Rais Samia anatarajiwa pia kukutana na Wakuu wa Nchi nyingine na viongozi wa Mashirika ya Kimataifa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya Tanzania na nchi na taasisi zao.
Post a Comment