Featured

    Featured Posts

RAIS SAMIA ATAJA FAIDA LUKUKI ZA SENSA YA WATU NA MKAZI YA 2022, ASEMA MOJAWAPO NI KUSAIDIA KUCHOCHEA BENKI KUTOA MIKOPO, KUPUNGUZA RIBA

Na CCM Blog, Dodoma
Rais Samia Samia Suluhu Hassan, amesema Sensa ya Watu na Makazi ina lengo la kufahamu idadi ya watu, mahali walipo, jinsia, rika, elimu, ajira, shughuli, makazi yao, mahali yalipo na hali yake na ili Serikali ifahamu wastani wa ongezeko la idadi ya watu katika nchi, hali ya uhamiaji kutoka vijijini kwenda mijini na kuwezesha nchi kutambua hatua mbalimbali za kimaendeleo.

Aamesema  kwamba Sensa inasaidia Serikali kufanya maamuzi kuhusu ugawaji wa rasilimali za Taifa na kupeleka huduma mbalimbali za jamii kwa wananchi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu kwenye maeneo yao kulingana na idadi ya watu na mahitaji.

Rais Samia Suluhu Hassan, amesema hayo leo tarehe 14 Septemba, 2021 wakati akihutubia na kuzindua Mkakati wa Uelimishaji na Uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Amesema kupitia madodoso ya Sensa hiyo itawezesha kutambua idadi ya majengo na mahali yalipo, itawezesha kufahamu hali ya mahitaji ya makazi nchini na kufahamu na kupanga mitaa kupitia anuani za makazi ambazo zitachochea benki kutoa mikopo na kupunguza viwango vya riba.

Rais amewaomba viongozi wa Serikali,Dini na vyama vya siasa kusisitiza wananchi kushiriki kikamilifu kwenye zoezi hilo la Sensa  ya Watu na Makazi.Pia amewasihi viongozi hao Dini wasisahau kuzungumzia sula la Sensa kila watakapokuwa wakitoa mahubiri kwa waumini wao.

Ameishukuru na kuipongeza Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa kwa kukamilisha mkakati wa Uelimishaji na Uhamasishaji Sensa mapema na kuwataka kwenda kuutekeleza.

Tukio hilo la uzinduzi limehudhuriwa pia na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Dkt. Khalid Salim Mohamed, Mawaziri, Manaibu Mawaziri, viongozi wa Dini pamoja na  vyama vya siasa. 

Rais Samia Suluhu Hassan, akibofya kitufe kuzindua Mkakati wa Uelimishaji na Uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, leo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana