Featured

    Featured Posts

SHAKA ATATUA MGOGORO WA ARDHI KWA NUSU SAA TU MTWARA, LEO

Ziara ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka mkoani Mtwara, imeleta neema, baada kiongozi huyo kufanikiwa kutatua ndani ya nusu saa, Mgogoro wa mpaka kati ya makazi ya Wananchi wa Mtaa wa Mtawanya Kata ya Mangamba Wilaya ya Mtwara Mjini na Eneo la Uwanja wa Ndege Mtwara uliodumu tangu mwaka jana. 

Shaka amefanikiwa kuutatua mgogoro huo kwa kutumia umakini wake alipowasili katika eneo hilo na kuzungumza na pande zote zinazohusika hadi kuhakikisha maamuzi yameafikiwa na pande zote mbili. 

Kufuatia hatua hiyo Wananchi wamemshukuru Shaka na kumpongeza Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka viongozi walio imara na makini na wanaojali wananchi ndani ya Chama na Serikali anayoingoza. 

Shaka amefika kufanya ziara Mtwara mjini ikiwa ni Sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo kutembelea kikazi mikoa minne ukiwemo wa Mtwara ambapo katika ziara hiyo Chongolo ameambatana na Sekretarieti ya CCM Taifa. Msikilize Shaka akizungumza. 
Tafadhali, BofyaHapo👇🏻

 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana