Featured

    Featured Posts

GF TRUCKS & EQUIPMENTS WAKUBALIANA NA WACHIMBAJI WADOGO GEITA KUSHIRIKIANA KIBIASHARA

Na Mwandishi Maalum, Geita
Uchimbaji madini hapa nchini ni miongoni mwa sekta muhimu ambazo zimekuwa zikitoa mchango kwa Taifa la Tanzania na pia kuchangia kwa namna moja au nyingine katika kukuza ajira kwa wananchi hasa vijana.

Lakini licha ya sekta hiyo ya madini kuonekana kufanya vizuri katika pato la taifa na ajira kwa wananchi hasa vijana, bado sekta hiyo inakumbwa na changamoto mbalimbali zinazokwamisha kufikiwa malengo yanayolingana na umuhimu wa sekta hiyo.

Pamoja na kuwepo changamoto kadhaa, lakini mojawapo ambayo ipo hasa kwa wachimbaji wadini wadogo ni wengi wao kuwa na vifaa duni na wengine kutokuwa navyo, jambo ambalo linasababisha uchimbaji wao kutotoa tija inayotakiwa.

Moja ya hatua za kuwezesha kuokoa hali hiyo ya wachimbaji wadogo kuwa na vifaa duni au kutokuwa navyo kabisa hasa vya kisasa ni wadau kujitokeza na kuwasaidia kwachimbaji hao kupata vifaa vya uchimbaji madini kwa njia za mikopo.

Kampuni ya GF Trucks & Equipments ambayo ni mahiri katika uuzaji wa mitambo ya kuchimbia madini na magari ya mizigo nchini imejitokeza kuwa mdau wa kuwasaidia wachimbaji wadogo ili kuwaondoa katika adha ya ukosefu wa vifaa vya uchimbaji madini.


Kapuni hiyo ya GF Tucks & Equipments katika imeingia mkataba wa ushirikiano wa kibiashara na wachimbaji wadogo mkoani Geita, Wakati Maonyeso ya Madini yaliyokuwa yakifanyika wiki iliyopita mkoani humo.

Pamoja na dhanira yake, pia inaonyesha Kampuni hiyo ilifikia hatua hyo hasa baada ya kuguswa na kauli ya Waziri  Mkuu Kassimu Majaliwa aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Maonyesho hayo ambapo aliwataka wawekezaji kuwakopesha au kuwapatia mikopo nafuu ya Mashine au Mitambo ya kufanyia kazi migodini  badala ya pesa kitu ambazo kwa mchimbaji sio kipaumbele'

Kwa kuzingatia hilo Kampuni ya Gf  inayouza Mitambo ya migodini ya XCMG pamoja na magari ya mizigo ya FAW ilishusha neema kwa kuingia makubaliano ya kufanya kazi pamoja na Umoja wa wachimbajin madini Wadogo wadogo mkoani Geita (GEREMA).

Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano  hayo na GEREMA Mkurugenzi wa Kampuni ya Gf Salman Karmal alisema Kutokana na kampuni hiyo kujikita katika uuzaji wa mitambo ya migodini na wadau wakuu ni wachimbaji wadogo kampuni hiyo imeona kuna haja ya kuingia mkataba wa kindugu baina na GEREMA.

"Leo hii tunafugua ukurasa mwingine kwa kusaini makubaliano ya ushirikiano wa kufanya  kazi pamoja na wachimbaji wadogo wa madini ambao ni wanachama wa GEREM, kupitia mkataba huu Mwanachama wa Umoja wa wachimbaji hawa ataweza kuingia katika familia ya  ya GF na kupata mkopo wa mitambo na maroli, bila kuwa na mashariti magumu, wala riba, sifa kubwa itakuwa ni yeye awe katika Chama hicho tu.

Tunajua wachimbaji wadogo hawana uwezo wa kununua mitambo ya kuchimbia  ili kukidhi mahitaji kwa kulitambua hilo kuanzia leo wachimbaji hao wadogo wanaweza kukopeshwa Mitambo, Magari kwa vigezo vidogo ambavyo hapo awali walikua hawana uwezo huo", alisema Karmal.

Kwa upande wake Katibu wa GEREMA Golden Hainga alisema mpango huo utaleta manufaa na tija kubwa kwa wachimbaji ambao hawana mitaji na hivyo kujikuta wakifanyakazi kwenye mazingira magumu yasiyo na tija na wakati mwingine kupata hasara.

“Utaratibu huu wa GF Truck ni mkombozi kwetu sisi mchimbaji mdogo maana hawa wataweka dhamana na Benki itatoa fedha, wachimbaji wamekua na kilio kwa miaka mingi wakiomba kukopeshwa vifaa au fedha ujio wa hawa wadau utasaidia hata mabenki kuwa na imani na wachimbaji", alisema Hainga.

Naye Mkuu wa mkoa wa Geita Rosemary Senyamule alisema lengo la Maonyesho ya Madini ni kuwakutanisha wachimbaji na wadau mbalimbali ambao kwa njia moja ama nyingine watajenga ushirikiano baina yao na wachimbaji na ilivyotokea kwa Kampuni ya GF na GEREMA.

Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wachimbaji wanaopatiwa mkopo kurudisha kwa wakati ili kujenga imani kwenye Taasisi  za fedha ambazo hadi sasa zinahofu kuwaamini wachimbaji wadogo katika suala la kuwapatia mikopo.

Alikaribisha Kampuni ya GF na wadau wengine kuwatembelea Wachimbaji wadogo ili kutambua changamoto wanazokaliliana naza ili kuwasaidia.

Mkuu wa mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule (katikati) akishuhudia  ubadilishanaji nyaraka kati ya Mkurugenzi wa Kampuni ya GF Trucks & Equipments Ltd, Salman Karmal (kushoto) na Katibu wa Chama cha Wachimbaji wadogo mkoani Geita(GEREMA) Golden Hainga,  baada ya kusaini makubaliano ya awali ya kushirikiana kati ya GF na GEREMA  wakati wa maonyesho ya Madini mkoni Geita  wiki iliyopita.

Mkuu wa mkoa wa Geita Rosemary Senyamule (katikati) akishuhudia Mkurugenzi wa kampuni ya GF Trucks & Equipments Ltd Salman Karmal (kushoto) na Katibu wa Chama cha Wachimbaji Wadogo mkoani Geita (GEREMA) Golden Hainga wakionyesha nyaraka  baaada ya kusaini makubaliano ya awali ya kushirikiana kati ya GF na GEREMA, wakati wa maonyesho ya Madini mkoni Geita.
Mkuu wa mkoa wa Geita Rosemary Senyamule (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mpango wa Kampuni ya GF kuwapatia mitambo  ya migodini na Magari ya mizigo Chama cha Wachimbaji wadogo mkoani Geita (GEREMA) ambapo mmpja ya wanachama wa GEREMA amenufaika na mpango huo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana