Nyumbu wakiwa Hifadhi ya Taifa Tarangire
Muongoza Watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Florence Shimbi akielezea tabia ya mnyama Nyumbu ambaye akili yake ni sifuri, yaani hana kumbukumbu lakini ana uwezo mkubwa wa kunusa kwa umbali dalili za mvua. Nyumbu humtegemea sana Pundamilia ambaye ana kumbukumbu hivyo humuongoza njia Nyumbu wakati wa kuhama.
Septemba 16,2021 nilibahatika kutembelea hifadhi hiyo nikiwa na viongozi wa Chama cha Skauti wa Kike cha Tanzania Girl Guides (TGGA) na kuzungumza na Mtalaam Florence ambaye alikuwa na mambo mengi ya kutuelezea kuhusu tabia za wanyama na ndege, miongoni mwao uhusiano uliopo kati ya Nyumbu na Pundamilia. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Nyumbu wakiwa karibu na Pundamilia Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video hapa chini, Mtaalamu Florence akielezea kuhusu tabia ya Nyumbu.....
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
Post a Comment