Featured

    Featured Posts

RAIS DK. MWINYI AMTUMIA SALAM ZA POLE RAIS MSTAAFU DK. SHEIN KUFUATIA KIFO CHA KAKA YAKE

Ikulu, Durban, Afrika Kusini

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za pole kwa Rais Mstaafu Dk. Ali Mohamed Shein kufuatia kifo cha Kaka yake Mzee Shein Mohamed Shein kilichotokea jana Novemba 14, 2021.


Katika salamu hizo za pole, Rais Dk. Mwinyi ambaye yupo Durban, nchini Afrika Kusini akisihiri ufunguzi wa Mkutano wa Maonesho ya Kukuza Biashara baina ya nchi za Afrika, ameeleza kusikitishwa kwake na kifo hicho na kumtakia pole na ustahamilivu Rais Mstaafu Dk. Shein yeye na familia yake katika kipindi hiki kigumu cha msiba.


"Rais Dk. Mwinyi na familia yake wamemuomba Mwenyezi Mungu amjaalie Marehemu Mzee Shein Mohamed Shein amlaze mahali pema peponi, Amin", imesema taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Ikulu leo Novemba 15, 2021.




author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana