Meneja wa Huduma na Uhusiano wa NHC, Bw.Muungano Saguye akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam. Meneja wa Huduma na Uhusiano wa NHC, Bw.Muungano Saguye akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ofisi za Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki na Masoko NHC, Bw.Elias Msese akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ofisi za Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
*******************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limeanza kuyafanyia mapitio madeni ya kodi na kuyahakiki ili kubainisha kila mdaiwa na mahali alipo ili mwezi Januari Shirika lianze kampeni kabambe ya ukusanyaji madeni hayo.
Ameyasema hayo Meneja wa Huduma na Uhusiano wa NHC, Bw.Muungano Saguye wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Shirika hilo Jijini Dar es Salaam Desemba 30,2021.
Amesema hadi sasa NHC inadai malimbikizo ya kodi ya jumla ya shilingi Bilioni 26 kutoka kwa wapangaji wake, hivyo Shirika limeanza kufanyia mapitio madeni hayo na kuyahakiki.
Aidha Bw.Saguye amesema malimbikizo hayo ya Shilingi Bilioni 26, yana uwezo wa kujenga nyumba nyingine 450 ambazo zitawasaidia watanzania wengine kupata makazi kupitia Shirika hilo.
“Mpaka sasa tumeshaanza mazungumzo na baadhi ya wadaiwa zikiwemo taasisi za serikali, kufikia Januari shirika litaanza mpango wa kukusanya madeni yake yote, hayo ni maelekezo ya serikali na bodi kwa wapangaji wasio waaminifu,” amesema.
Amesema kuwa shirika limebaini wapangaji wasio halali wanaoishi kwenye nyumba kinyume na utaratibu wapatao 30 na tayari wamewachukulia hatua za kisheria kwa kuwanyang’anya upangaji na kuwapatia wanaostahili.
Pamoja hayo amesema kuwa Shirika limetenga Shilingi bilioni 8.5 kwa mwaka huu wa fedha kukarabati majengo yake 350 ambapo mpaka sasa limeshaanza ukarabati wa baadhi ya majengo katika mkoa wa Kilimanjaro na Dar es Salaam.
Post a Comment