Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Dodoma.
Kanisa Halisi la Mungu Baba lenye Makao yake Makuu Tegeta Namanga Jijini Dar es Salaam, linatarajiwa 'kuliteka' Jiji la Dodoma na Viunga vyake, litakapokuwa likifanya Mkutano Mkubwa wa Ibada ya kuliombea Taifa Amani na Utulivu leo Jumapili Januari 16, 2022 (12 Kilsleu 1) mchana, katika Uwanja wa Jamhuri mjini hapa.
Mkutano huo ambao utafanyika katika Uwanja huo wa Jamhuri kuanzia saa 8 mchana hadi saa 10 jioni, utakuwa ni wa kuhitimisha Ibada ya siku 10 kwa ajili ya Matunda (Sadaka) kwa ajili hiyo ya kuliombea Taifa Amani na Utulivu ambayo ilianza Januari 7, 2022 (3 Kiselu 1).
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, Baba Halisi amesema Ibada hiyo itakuwa ya kipekee tofauti na ibada za kawaida na kuwataka Watu wote bila kubagua, kufika kwenye Mkutano huo akisema, "Njoo mkononi na matunda (sadaka) ya kusimamisha Amani na Utulivu, maana ni ibada maalum kwa ajili ya Taifa zima".
Kwa kuzingatia kuwa ni Ibada Maalum kwa ajili ya Taifa zima, Baba Halisi amewaomba wale ambao hawatapata nafasi ya kufika Uwanjani kwenye Ibada hiyo kwa sababu ya majukumu waliyonayo wapeleke matunda (sadaka) yao Tanzania Commercial Bank A/C No 172405000002 na kwamba watabarikiwa kama yule aliyefika Uwanjani ila watakaofanya hiyo wataarifu kupitia simu namba 0746001119.
Ibada hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na Uzao (Waumini) kutoka mikoa yote hapa Nchini na pia itahudhuriwa na Makuhani kutoka ndani na nje ya Tanzania, na inatarajiwa kuhudhuriwa pia na viongozi na wananchi mbalimbali wa kawaida ili kushuhudia ibada hiyo ya kipekee.
Post a Comment