Katika Mkutano wake wa 145 uliofanyika tarehe 13 Januari, 2022, Baraza la Mitihani
la Tanzania liliidhinisha kutangazwa rasmi kwa matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa
Darasa la Nne (SFNA), Kidato cha Pili (FTNA), Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE)
na Maarifa (QT) iliyofanyika mwezi Oktoba, Novemba na Desemba, 2021.
2.0 USAJILI NA MAHUDHURIO
2.1 Upimaji wa Darasa la Nne (SFNA)
Jumla ya wanafunzi 1, 681,791 walisajiliwa kufanya Upimaji wa Darasa la Nne
wakiwemo wasichana 856,860 sawa na asilimia 50.95 na wavulana 824,931
sawa na asilimia 49.05. Kati ya wanafunzi waliosajiliwa, wanafunzi 1,561,599
walifanya Upimaji, wakiwemo wasichana 808,047 (94.30%) na wavulana
753,552 (91.35%). Wanafunzi 120,192 (7.15%) hawakufanya Upimaji, kati
yao wasichana ni 48,513 (5.70%) na wavulana ni 71,379 (8.65%).
2.2 Upimaji wa Kidato cha Pili (FTNA)
Jumla ya wanafunzi 652,611 walisajiliwa kufanya Upimaji wa Kidato cha Pili
wakiwemo wasichana 348,198 sawa na asilimia 53.35 na wavulana 304,413
sawa na asilimia 46.65. Kati ya wanafunzi waliosajiliwa, wanafunzi 602,955
walifanya Upimaji, wakiwemo wasichana 326,664 (93.82%) na wavulana
276,291 (90.76%). Wanafunzi 49,656 (7.61%) hawakufanya Upimaji, kati yao
wasichana ni 21,534 (6.18%) na wavulana ni 28,122 (9.24%).
2.3 Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE)
(a) Watahiniwa Wote (Shule na Kujitegemea)
Jumla ya watahiniwa 538,024 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato
cha Nne wakiwemo wasichana 285,010 (52.97%) na wavulana
253,014 (47.03%). Kati ya watahiniwa 538,024 waliosajiliwa,
watahiniwa wa shule walikuwa 501,039 na watahiniwa wa kujitegemea
walikuwa 36,985.
(b) Watahiniwa wa Shule
Kati ya watahiniwa 501,039 wa shule waliosajiliwa, watahiniwa 487,730
sawa na asilimia 97.34 walifanya mtihani ambapo wasichana walikuwa
256,415 (97.17%) na wavulana 231,315 (97.54%). Watahiniwa 13,309
sawa na asilimia 2.66 hawakufanya Mtihani.
(c) Watahiniwa wa Kujitegemea
Kati ya watahiniwa 36,985 wa kujitegemea waliosajiliwa, watahiniwa
33,621 sawa na asilimia 90.90 walifanya mtihani na watahiniwa 3,364
sawa na asilimia 9.10 hawakufanya Mtihani.
2.4 Mtihani wa Maarifa - QT
Jumla ya watahiniwa 9,874 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Maarifa wakiwemo
wasichana 5,402 sawa na asilimia 54.71 na wavulana 4,472 sawa na asilimia
45.29. Kati ya Watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa 8,324 walifanya Mtihani
wa Maarifa, wakiwemo wasichana 4,619 (85.51%) na wavulana 3,705
(82.85%). Watahiniwa 1,550 (15.70%) hawakufanya Mtihani, kati yao
wasichana ni 783 (14.49%) na wavulana ni 767 (17.15%).
3.0 MATOKEO YA UPIMAJI/MTIHANI
3.1 Upimaji wa Darasa la Nne (SFNA)
(a) Ufaulu wa Jumla
Takwimu za matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne
zinaonesha kuwa jumla ya wanafunzi 1,347,554 kati ya wanafunzi
1,561,516 wenye matokeo ya Upimaji sawa na asilimia 86.30
wameweza kupata ujuzi na maarifa ya kuwawezesha kuendelea na
Darasa la Tano, ambapo wasichana ni 708,203 (87.65%) na wavulana
ni 639,351 (84.85%). Aidha, wanafunzi 213,962 sawa na silimia 13.70
wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na Darasa la
Tano.
Mchanganuo wa ufaulu kwa madaraja mbalimbali umeoneshwa katika
Jedwali la 1.3
Jedwali la 1: Mchanganuo wa Ufaulu kwa Madaraja (SFNA)
KIWANGO
CHA UFAULU
IDADI %
DARAJA
LA
WASTANIME KE JUMLA
Mzuri sana 34,665 33,075 67,740 4.34 A
Mzuri 157,615 159,803 317,418 20.33 B
Wastani 271,960 316,456 588,416 37.68 C
Unaridhisha 175,111 198,869 373,980 23.95 D
Usioridhisha 114,161 99,801 213,962 13.70 E
(b) Mchanganuo wa ufaulu Kimasomo
Takwimu za matokeo zinaonesha kuwa wanafunzi wa Darasa la Nne
2021 wamefanya vizuri kwa masomo yote ambapo ufaulu wa chini ni
asilimia 69.41 kwa somo la Hisabati na ufaulu wa juu ni 91.33 kwa
somo la Maarifa ya Jamii kama ilivyoainishwa katika Jedwali la 2.
Jedwali la 2: Mchanganuo wa Ufaulu Kimasomo (SFNA)
SOMO WENYE
MATOKEO
WALIOFAULU
IDADI %
KISWAHILI 1,560,360 1,326,573 85.02
ENGLISH LANGUAGE 1,560,876 1,138,452 72.94
MAARIFA YA JAMII 1,560,797 1,425,478 91.33
HISABATI 1,560,611 1,083,166 69.41
SAYANSI NA TEKNOLOJIA 1,560,556 1,369,606 87.76
URAIA NA MAADILI 1,560,759 1,423,379 91.20
(c) Wanafunzi 10 Bora Kitaifa
Wanafunzi 10 Bora Kitaifa katika Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne
(SFNA) 2021 wameanishwa katika Jedwali la 34
Jedwali la 3: Wanafunzi Kumi (10) Bora Kitaifa (SFNA)
NAFASI JINA JINSI SHULE MKOA
1 JOEL LUBANGO LEONARD M LIBERMANN DAR ES SALAAM
2 FALIMA JOSEPH MWENURA M GREEN STAR
JUNIOR
SHINYANGA
3 GOODLUCK MTAKI
GAMBACHALA
M GREEN STAR
JUNIOR
SHINYANGA
4 CAREEN SIMON SLAA F SASA ARUSHA
5 JOYCE JOHN NDONDE F WONDER KIDS LINDI
6 SAMIRAH JAFARI MNALI F WONDER KIDS LINDI
7 JONATHAN JOSEPH MAZIKU M GREEN STAR
JUNIOR
SHINYANGA
8 BALKIS HAMISI MAJOWE F WONDER KIDS LINDI
9 CHRISTOPHER NICHOLAUS
KILEO
M GREEN STAR
JUNIOR
SHINYANGA
10 DOREEN PAUL SANARE F ST. FRANCIS
DE SALE
ARUSHA
(d) Mpangilio wa Shule kwa Ubora wa Ufaulu
Takwimu za matokeo zinaonesha Shule 10 zilizofanya vizuri zaidi
Kitaifa zimeainishwa katika Jedwali la 4
Jedwali la 4: Shule Kumi (10) Bora Kitaifa (SFNA)
NAFASI NAMBA JINA LA SHULE IDADI MKOA
1 PS0904095 TWIBHOKI 43 MARA
2 PS0904122 GRAIYAKI 45 MARA
3 PS0504112 ST PETER CLAVER 49 KAGERA
4 PS1701125 GREEN STAR JUNIOR 45 SHINYANGA
5 PS1701035 KWEMA MODERN 42 SHINYANGA
6 PS1601158 KIKODI 42 RUVUMA
7 PS0504008 BOHARI 89 KAGERA
8 PS1701064 ROCKEN HILL 45 SHINYANGA
9 PS1304104 MUSABE 107 MWANZA
10 PS0201096 MTUKI HIGHLAND 43 DAR ES SALAAM5
3.2 Upimaji wa Kidato cha Pili (FTNA)
(a) Ufaulu wa Jumla
Takwimu za Matokeo ya Upimaji wa Kidato cha Pili zinaonesha kuwa,
jumla ya wanafunzi 555,857 (92.32%) kati ya wanafunzi 602,107 wenye
matokeo ya Upimaji wamepata Ujuzi na Maarifa ya kuwawezesha
kuendelea na Kidato cha Tatu, ambapo wasichana ni 300,492 (92.11%)
na Wavulana ni 255,365 (92.57%). Mwaka 2020 wanafunzi 550,979
sawa na asilimia 91.61 walipata alama za kuwawezesha kuendelea na
masomo ya Kidato cha Tatu. Hivyo, ufaulu wa Kidato cha Pili (FTNA)
umepanda kwa asilimia 0.71 ukilinganishwa na mwaka 2020.
(b) Mchanganuo wa Ufaulu Kimasomo
Takwimu za matokeo ya Upimaji wa Kidato cha Pili zinaonesha kuwa
wanafunzi wamefanya vizuri zaidi katika masomo ya Civics, Geography,
Kiswahili, English Language, Biology na Book-keeping ambapo ufaulu
wa masomo hayo upo juu ya wastani kati ya asilimia 51.98 na 95.21.
Aidha, takwimu za matokeo zinaonesha kuwa wanafunzi hawakufanya
vizuri katika masomo ya History, Physics, Chemistry, Basic Mathematics
na Commerce ambapo Ufaulu wake upo chini ya wastani kati ya asilimia
19.52 na 49.77.
Mchanganuo wa ufaulu kwenye masomo ya msingi umeainishwa katika
Jedwali la 5.
Jedwali la 5: Ufaulu katika Masomo ya Msingi
SOMO UFAULU (%)
CIVICS 71.13
HISTORY 49.77
GEOGRAPHY 52.30
KISWAHILI 95.21
ENGLISH LANGUAGE 86.49
PHYSICS 31.03
CHEMISTRY 42.37
BIOLOGY 51.98
BASIC MATHEMATICS 19.52
COMMERCE 46.39
BOOK KEEPING 70.616
(c) Wanafunzi 10 Bora Kitaifa
Wanafunzi 10 Bora katika Upimaji wa Kitaifa Kidato cha Pili 2021
wameanishwa katika Jedwali la 6:
Jedwali la 6: Wanafunzi Kumi (10) Bora Kitaifa
NAFASI JINA JINSI SHULE MKOA
1 GEOVIN STEVEN MACHA M JUDE ARUSHA
2 MOSES WILLIAM MASOME M HERITAGE PWANI
3 PIUS FULGENCE TAIRO M TENGERU
BOYS'
ARUSHA
4 HENRY REVOCATUS
SHELEMBI
M JUDE ARUSHA
5 SHILANGA EMMANUEL
MALEGI
M HERITAGE PWANI
6 LOI MARTIN KITUNDU F FEZA GIRLS' DAR ES SALAAM
7 JOSHUA EDMUND LEO M TENGERU
BOYS'
ARUSHA
8 BRIAN FELIX CHILLE M MARIAN
BOYS'
PWANI
9 CORNEL JOSEPH KAROLI M JUDE ARUSHA
10 ELIZABETH PETER MSENGI F ST.MONICA
MOSHONO
GIRL'S
ARUSHA
(d) Mpangilio wa Shule kwa Ubora wa Ufaulu
Takwimu za matokeo zinaonesha Shule 10 zilizofanya vizuri zaidi Kitaifa
kwenye Upimaji wa Kidato cha Pili zimeainishwa katika Jedwali la 7
Jedwali la 7: Shule Kumi (10) Bora Kitaifa
NAFASI JINA LA SHULE IDADI MKOA
1 ST. FRANCIS GIRLS' 92 MBEYA
2 KEMEBOS 73 KAGERA
3 GRAIYAKI 65 MARA
4 CANOSSA 99 DAR ES SALAAM
5 TENGERU BOYS' 138 ARUSHA
6 ST.MONICA MOSHONO GIRL'S 93 ARUSHA
7 ST.AUGUSTINE TAGASTE 159 DAR ES SALAAM
8 CENTENNIAL CHRISTIAN 185 PWANI
9 BETHEL SABS GIRLS’ 96 IRINGA
10 BRIGHT FUTURE GIRLS’ 144 DAR ES SALAAM7
3.3 Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE)
(a) Ufaulu wa Jumla
Jumla ya Watahiniwa wa Shule 422,388 sawa na asilimia 87.30 kati ya
ya watahiniwa 483,820 wenye matokeo ya Kidato cha Nne wamefaulu.
Wasichana waliofaulu ni 218,174 sawa na asilimia 85.77 na wavulana ni
204,214 sawa na asilimia 89.00. Mwaka 2020 Watahiniwa 373,958 sawa
na asilimia 85.84 ya Watahiniwa wa Shule walifaulu mtihani huo. Hivyo,
ufaulu wa Watahiniwa wa Shule umeongezeka kwa asilimia 1.46
ikilinganishwa na mwaka 2020.
(b) Ubora wa Ufaulu
Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata Watahiniwa wa
Shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa
Madaraja ya I - III ni 173,422 sawa na asilimia 35.84 wakiwemo
wasichana 75,056 (29.51%) na wavulana 98,366 (42.87%). Mwaka 2020
watahiniwa waliopata ufaulu wa madaraja I – III walikuwa 152,909 sawa
na asilimia 35.10. Hivyo, ubora wa ufaulu umeongezeka kwa asilimia
0.74.
Mchanganuo wa ufaulu kwa kila daraja kwa Watahiniwa wa Shule
umeoneshwa katika Jedwali la 8.
Jedwali la 8: Ufaulu katika Madaraja
Daraja la
Ufaulu
Wavulana Wasichana Jumla
Idadi Asilimia Idadi Idadi Asilimia
I 19,153 8.35 12,623 4.96 31,776 6.57
II 34,856 15.19 25,419 9.99 60,275 12.46
III 44,357 19.33 37,014 14.55 81,371 16.82
I-III 98,366 42.87 75,056 29.51 173,422 35.84
IV 105,848 46.13 143,118 56.26 248,966 51.46
I-IV 204,214 89.00 218,174 85.77 422,388 87.30
Fail 25,231 11.00 36,201 14.23 61,432 12.70
(c) Mchanganuo wa Ufaulu Kimasomo
Takwimu za matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne zinaonesha kuwa
watahiniwa wamefanya vizuri katika masomo mengi ya msingi ambapo
ufaulu wa masomo hayo uko juu ya wastani kati ya asilimia 55.33 na8
95.58. Aidha, watahiniwa hawakufanya vizuri katika somo moja (01) la
Basic Mathematics, ambapo ufaulu wa somo hili upo chini ya wastani.
Mchanganuo wa ufaulu katika masomo ya msingi umeainishwa kwenye
Jedwali la 9.
Jedwali la 9: Ufaulu katika Masomo ya Msingi
SOMO UFAULU (%)
CIVICS 70.46
HISTORY 59.21
GEOGRAPHY 60.55
KISWAHILI 95.58
ENGLISH LANGUAGE 66.84
PHYSICS 55.33
CHEMISTRY 92.02
BIOLOGY 67.23
BASIC MATHEMATICS 19.54
COMMERCE 67.40
BOOK KEEPING 71.30
(d) Watahiniwa 10 Bora Kitaifa
Watahiniwa 10 Bora Kitaifa katika Mtihani wa Kitaifa Kidato cha Nne
(CSEE) 2021 wameanishwa katika Jedwali la Jedwali la 10.
Jedwali la 10: Watahiniwa Kumi (10) Bora Kitaifa (CSEE)
NAFASI JINA JINSI SHULE MKOA
1 CONSOLATA PROSPER
LUBUVA
F ST. FRANCIS GIRLS MBEYA
2 BHUTOI ERNEST NKANGAZA F ST. FRANCIS GIRLS MBEYA
3 WILIHELMINA STEVEN
MUJARIFU
F ST. FRANCIS GIRLS MBEYA
4 GLORY JOHN MBELE F ST. FRANCIS GIRLS MBEYA
5 MARY GEORGE NGOSO F ST. FRANCIS GIRLS MBEYA
6 HOLLY BEDA LYIMO F BRIGHT FUTURE
GIRLS
DAR ES SALAAM
7 BLANDINA KAREN CHIWAWA F ST. FRANCIS GIRLS MBEYA
8 IMAM SULEMAN MOGAEKA M FEZA BOYS' DAR ES SALAAM
9 MFAUME HAMISI MADILI M ILBORU ARUSHA
10 CLARA STRATON ASSENGA F ST. FRANCIS GIRLS MBEYA9
(e) Mpangilio wa Shule kwa Ubora wa Ufaulu
Takwimu za matokeo zinaonesha Shule 10 zilizofanya vizuri zaidi Kitaifa
zimeainishwa katika Jedwali la 11.
Jedwali la 11: Shule Kumi (10) Bora Kitaifa (CSEE)
NAFASI JINA LA SHULE IDADI MKOA
1 KEMEBOS 65 KAGERA
2 ST. FRANCIS GIRLS 92 MBEYA
3 WAJA BOYS 60 GEITA
4 BRIGHT FUTURE GIRLS 95 DAR ES SALAAM
5 BETHEL SABS GIRLS 78 IRINGA
6 MAUA SEMINARY 86 KILIMANJARO
7 FEZA BOYS' 62 DAR ES SALAAM
8 PRECIOUS BLOOD 92 PWANI
9 FEZA GIRLS' 64 DAR ES SALAAM
10 MZUMBE 102 MOROGORO
3.4 Mtihani wa Maarifa (QT)
Takwimu za matokeo ya Mtihani wa Maarifa (QT) zinaonesha kuwa jumla ya
watahiniwa 4,763 sawa na asilimia 57.23 ya watahiniwa 8,324 wenye
matokeo ya Mtihani wa Maarifa (QT) wamefaulu. Mwaka 2020 jumla ya
watahiniwa 4,446 sawa na asilimia 55.19 walifaulu mitihani wa Maarifa (QT),
hivyo ufaulu wa Mtihani wa Maarifa (QT) umepanda kwa asilimia 2.04.
4.0 MATOKEO YALIYOFUTWA
Baraza la Mitihani limefuta matokeo yote ya watahiniwa 214 waliofanya udanganyifu
katika upimaji/mtihani kwa mujibu wa Kifungu cha 5 (2) (i) na (j) cha sheria ya
Baraza la Mitihani sura ya 107 kikisomwa pamoja na Kifungu cha 30(2) (b) 2016 cha
Kanuni za Mitihani. Kati ya watahiniwa waliobainika kufanya udanganyifu watahiniwa
83 ni wa Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne (SFNA), 27 ni wa Upimaji wa Kitaifa
wa Kidato cha Pili (FTNA), 102 ni wa Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na
Watahiniwa 02 ni wa Mtihani wa Maarifa(QT).10
5.0 MATOKEO YALIYOZUILIWA
Baraza la Mitihani la Tanzania limezuia kutoa matokeo ya watahiniwa 555 ambao
walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya upimaji/mtihani kwa masomo yote
au idadi kubwa ya masomo. Watahiniwa husika wamepewa fursa ya kufanya
upimaji/mtihani kwa masomo ambayo hawakuyafanya kwa sababu ya ugonjwa
mwaka 2022 kwa mujibu wa Kifungu cha 32(1) cha Kanuni za Mitihani. Kati ya
watahiniwa waliopewa fursa ya kurudia upimaji/mitihani yao mwaka 2022,
watahiniwa 198 ni wa Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili (FTNA) na 357 ni wa
Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE).
6.0 PONGEZI ZA BARAZA
Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuchukua fursa hii kuzipongeza Kamati za
Uendeshaji Mitihani za Mikoa na Halmashauri/Manispaa, Wakuu wa Shule na vituo
vya mtihani, Wasimamizi na Wasahihishaji wa Mitihani na Upimaji iliyofanyika
Oktoba, Novemba na Desemba, 2021 kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya katika
kutekeleza jukumu la Uendeshaji Upimaji/Mitihani ya 2021.
7.0 UPATIKANAJI WA MATOKEO
Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne, Kidato cha Pili (FTNA), Mitihani ya
Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) iliyofanyika Oktoba, Novemba na Desemba,
2021 yanapatikana katika tovuti zifuatazo:
www.matokeo.necta.go.tz,
www.necta.go.tz,
www.tamisemi.go.tz,
Dkt. Charles E. Msonde
KATIBU MTENDAJ
Post a Comment