Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Dkt Edmund Mndolwa akionesha ufunguo baada ikiwa ni ishara ya kukabidhiwa jengo la Makao Makuu ya umoja huo jijini Dodoma. Jengo hilo limekarabatiwa na Kampuni tanzu ya Umoja huo ya Jitegemee kwa gharama ya zaidi ya sh. mil. 200. Sehemu ya fedha hizo zimetolewa na CCM Makao Makuu kusaidia kukamilisha ukarabati huo.
Dkt. Mndolwa akioneshwa moja ya vyumba vilivyokaratabiwa.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Jitegemee, Yainabu Juma akisoma taarifa ya ukarabati wa jengo hilo lililopo eneo la Mji mpya karibu kabisa na Makao Makuu ya CCM .
Viongozi wa Umoja wa Wazazi, wakiwa na walimu pamoja na wahasibu wa shule za umoja huo nchini ambao wapo Dodoma katika kikao kazi cha kupanga mkakati wa kuboresha shule hizo.
Dkt Mndolwa akitia saini kwenye nyaraka ya ukarabati wa jengo hilo.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Jitegemee,Martha Uleka akitia saini kwenye nraka hizo.
Katibu Mku wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Gilbert Kalima naye akitia saini kwenye nyaraka hizo.
Katibu Mkuu, Kalima akiangalia moja ya samani zitakazowekwa katika jengo hilo.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
JUMUIYA ya Wazazi imekabidhiwa jengo lake lililopo katika eneo la Mji Mpya Dodoma mara baada ya kukamilika kwa ukarabati uliokuwa ukifanywa na Kampuni ya Jitegemee Trading Company Limited, Januari 15,2022.
Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano hayo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Dkt. Edmund Mndolwa amesema kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia sana kurahisisha utendaji wa Jumuiya hiyo, pia ametoa shukrani zake za dhati kwa Chama Cha Mapinduzi hususani Katibu Mkuu Ndugu Daniel Chongolo.
“Nichukue fursa hii kushukuru Chama Cha Mapinduzi hususani Katibu Mkuu Bwana Chongolo kwa ushirikiano aliotuonyesha”
Dkt. Mndolwa pia alieleza kuwa uzinduzi rasmi wa jengo hilo utatangazwa na mgeni rasmi wa uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Awali akitoa maelezo ya ukarabati wa jengo hilo ambalo lilikuwa la ghorofa moja, Meneja wa Kampuni ya Jitegemee Ndugu Zainabu Juma alisema gharama kuu za ukarabati huo ni Tshs. 230,806,705.
Viongozi mbali mbali walishiriki makabidhiano hayo akiwemo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Bw. Gilbert Kalima, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya (Zanziba) Ndg. Othman Maulid, Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Jitegemee Ndugu Martha Uleka, Walimu Wakuu wa Shule za Jumiya pamoja na Viongozi nawadau wengine mbalimbali.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video ujue yaliyojiri wakati wa makabidhiano hayo....
ReplyForward
|
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
Post a Comment