Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Skauti wa Kike Tanzania,TGGA Taifa, Consolatha Shayo ameyafunga rasmi mafunzo ya kuwajengea uwezo wa uelewa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi na jinsi ya kukabiliana nayo.Mafunzo hayo yaliyohudhuriwa na viongozi wa wa TGGA wa mikoa 12 na viongozi kutoka nchi za Benin na Lesotho zamefanyika kwa siku 5 katika Barza la Maaskofu (TEC) Kurasini jijini Dar es Salaam.Pia walikuwepo wakufunzi wa kujitolea kutoka Chama cha Skauti wa Kike Duniani (WAGGGS).
Makamu Mwenyekiti wa TGGA, Consolatha akimkabidhi mtoto pekee Mysam Ameri aliyehudhuria mafunzo hayo. Ni mwanachama wa TGGA ngazi ya Tanzanite.
Consolatha akikabidhi vyeti kwa viongozi waliohudhuria mafunzo hayo.Consolatha akiwakabidhi zawadi ya kalenda ya TGGA wakufunzi wa kujitolea kutoka WAGGGS na GLACC.
Meneja wa Programu ya Mabadiliko ya Tabianchi wa TGGA, David Mbumila akikabidhiwa zawadi na Meneja wa Programu ya GLACC, Pascaline Umulisa (kushoto).
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Consolatha akifunga mafunyo hayo na Pascaline Umulisa akitoa shukrani....
Post a Comment