***********************
Adeladius Makwega
Dodoma.
Kama nilivyokueleza awali kuwa baadhi ya koo za Wajita kama vile Wabalinga na Wabakome walipita eneo la Ukerewe kabla ya kufika huko Majita na kuweka makazi yao. Ndiyo kusema kuwa hata Wakerewe wana mahusiano makubwa mno na Wajita.
Hivi sasa Makao Makuu ya serikali yapo Dodoma jambo hilo lina athari kubwa jwa jamii ya Wagogo kwani kuhamia huko kwa makao makuu wagogo wengi watazaliana na wageni hivyo pengine Dodoma kuwa ni Jiji la makabila mchanganyiko kama ilivyo Dar es Salaam. Sawa na mataifa yenye watu mchanganyiko (cosmopolitan).
Mwanakwetu naomba niende mbali zaidi katika hili, kwa mfano mimi binafsi baba yangu alitoka Mbagala Dar es Salaam na kuja Dodoma katika Oparesheni vijiji vya Ujamaa na huko akakutana na mama yangu na mimi kuzaliwa, Mpwapwa.
Kwa mtazamo huo Wakerewe na Wajita ni ndugu, kukiwa na hoja kuwa Wakerewe hao wametokea Bukoba.
Lugha ya Kijita na Kikerewe zimekuwa na mfanano mkubwa mno, ikiaminika kuwa Wajita na Wakerewe wote wana asili moja katika baadhi ya koo. Kukiwa na hoja kuwa Wakerewe waliwafurusha Wajita katika kisiwa chao kwa kuwa Wajita walipenda mno kula ndizi. Wakererwe waliwachukua Wajita watunze mashamba ya ndizi zilipoiva Wajita wakala ziote. Shida hiyo ilisababisha Wakerewe kukasilika na kuwaadhibu kwa kuwakata vichwa. Jambo hilo hilo likababisha ugomvi na ndipo Wajita wakaondoka katika visiwa hivyo vya Ukerewe.
Wakiamini kuwa Wajita si welevu na mabingwa wa kula huku wakimalizwa kama vile mgomba wa ndizi kuwa ndizi ikikomaa wanaikata na mgomba kutupwa huko. Maelezo haya yanaungwa mkono na E.S Gesase katika maandiko yako ya utamaduni.
Wajita walikuwa Majita walikuwa wakipita Ukerewe na kwenda kutafuta vyuma huko Uzinza huku Wakerewe wakiwasumbua mno.
“Mgooro huo ulisababisha Chifu wa Wajita anayefahamika kama Kusaga na Chifu wa Wakerewe Machunde kujenga udugu baina yao na kuondoa tofauti zao. Jambo hilo la kukubaliana kuondoa ugomvi lilikuwa jepesi kwa sababu moja kubwa kuwa Ukerewe yenyewe kulikuwa na ugomvi wa ndugu kwa ndugu uchifuni. Yaani Chifu Machunde na kaka yake alikuwa anafahamika kama Machumu.” Hilo linasisitizwa na G S Gesase.
Machumu alitaka kumpindua kaka yake Machunde ili yeye awe chifu, kwa usalama Chifu Machunde alikubaliana kupatana na Wajita ili awe marafiki wa kumlinda pale anapopata tatizo.
“Machumu aliendelea na nia hiyo aliposhindwa mapinduzi yake alikimbilia kwa Wajita ili kuwa salama kwa Chifu Kusaga. Chifu Machunde alimuomba chifu wa Wajita kumrudisha Machumu kwao na kweli Chifu Kusaga alifanya hivyo kwa kuwa walikuwa wamepatana. Machumu alikabidhiwa huko, huku macho yake yakiwa yameondolewa na jambo hilo lilikuwa ni kumpunguza nguvu na kuondoa vurugu akirudi Ukerewe.” Anaongeza G.S Gesase.
Jambo hio lilijenga udugu mkubwa kwa Wajita na Wakerewe wakawekeana nadhiri wakaondoa uadui na wakawa watani hadi leo hii. Huku wakitembeleana na kuona binafsi nina hakika wapo Watanzania wengi katika mikoa hiyo walizaliwa kutokana na maelewano ya makabila haya mawili.
Mwanakwetu kwa leo naishia hapo. Usikose kusoma matini ijayo ambapo nitamalizia sehemu ya mwisho ya kabila hili hususani Utani wa Wajita na Wakerewe.
Nakutakia siku njema.
makwadeladius@gmail.com
0717649257
Post a Comment