Mwenyekiti wa bodi kuu ya utendaji ya WHO Patrick Amoth ametoa taarifa hiyo katika mkutano wa bodi hiyo mjini Geneva ambako hatua ya Ghebreyesus ya kutaka kuwania muhula wa pili WHO imepangwa kujadiliwa.
Amoth amesema ombi la serikali ya Ethiopia ni suala gumu lenye kubeba athari za kisiasa na liko nje ya mfumo wa taratibu za kamati hiyo na kupendekeza suala hilo liwekwe kando, na kujadiliwa na wale wanaohusika katika wakati mwafaka.
Wanachama wote 34 wa WHO wa bodi hiyo wamekubaliana na mwelekeo uliotolewa.
Katibu mkuu wa WHO mwanzoni mwa mwezi huu alisema msaada unazuiwa kuingia katika jimbo la Tigray ambako ndiko alikotokea na ambako vikosi vya wapiganaji wa TPLF wanapambana na wanajeshi wa serikali kuu.
Post a Comment