Na Bashir Nkoromo, Tegeta
Maandalizi ya safari ya kwenda Hija ya Chanzo Halisi ya Kanisa Halisi la Mungu Baba, itakayofanyika mkoani Kigoma, tarehe 27 mwezi huu (26 Thebeti Majira Halisi) yamezidi kupamba moto baada Uzao (waumini) wa Kanisa hilo kuhamasika na kujitokeza kwa wingi kujiorodhesha ili kuhudhuria Hija hiyo.
Hamasa ya Uzao au waumini hao kujiorodhesha na kulipa nauli kwa ajili ya safari ya Hija hiyo, imekolezwa na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, Baba Halisi, baada ya kufafanua kwa kina maana halisi ya Hija hiyo, katika Ibada iliyofanyika leo, Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Namanda Jijini Dar es Salaam.
Mbali na kujiorodhesha Uzao wa Waumini kadhaa wa lioshiriki katika Ibada hiyo, wamejitokeza mbele ya Baba Halisi na kuwa tayari kuchangia gharama mbalimbali zitakazofanikisha Hija hiyo ya Chanzo Halisi, ikiwemo matangazo ya vyombo kadhaa vya habari na kuchapisha mabango.
Kabla ya kutoa ufafanuzi kuhusu kuhusu umuhimu kila mtu kushiriki, alisema Ibada kubwa ya Hija hiyo itafanyika katika Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma mjini kuanzia saa 8 mchana hadi saa 10 jioni, siku ya Jumapili ya tarehe hiyo ya 27, mwezi huu (26 Thebeti Majira Halisi) na itahudhuriwa hadi na watu kutoka Mataifa ya Marekani, Ulaya, Asia na Astralia.
"Sauti Mpya (2019) ambayo imetangaza kuwa Tanzania ni Taifa Baba ilisikika Kigoma, Tanzania, Sauti Mpya ambayo imetangaza kuwa Afrika ni Bara la Nuru ilisikika Kigoma, Tanzania; Sauti Mpya ambayo ni zaidi ya zile Sauti Saba ilisikika Kigoma,Tanzania, Sauti Mpya ambayo ni zaidi ya ishara tatu mbinguni (Ufunuo 12:1-9) ilisikika Kigoma, Tanzania na Sauti Mpya ambayo ni zaidi ya Nafsi ya Moyo (Miungu tisa mitakatifu iliyofafanuliwa ndani ya Kitabu) ilisikika pia Kigoma, Tanzania.
Sasa Kigoma, Tanzania na Afrika tujitambue kuwa tuna Sauti Mpya ambayo inabadilisha maisha mabaya kuwa mazuri. Sauti Mpya imebeba kila kitu kizuri. Hija hii ya Chanzo Halisi cha Mungu Baba inayofanyika Kigoma, siyo maigizo wala usanii, ni halisi", alisema Baba Halisi akifafanua umuhimu wa Hija hiyo na kwa nini inabidi ifanyike Kigoma kila mwaka na kuongeza kuwa Sauti hiyo mpya sasa imepokelewa katika mabara yote kwa utukufu wa Mungu Baba.
Baba Halisi amesema kutokana na sababu hizo Watu wa Dini zote, Madhehebu yote, Makabila yote, Lugha zote, Ngazi zote, Sekta zote na Mtaifa yote wanapaswa kuhudhuria Ibada hiyo ya Hija ya Chanzo Halisi bila kukosa.
"Sasa kwa kuwa kuanzia leo Tumejivua Moyo wa zamani, haitaitwa tena kutoa Sadaka bali Iitaitwa kutoa matunda", Akasema Baba Halisi wakati akitoa matunda yake kwenye chombo maalum, wakati wa Ibada hiyo.
Baada ya Baba Halisi kutoa madunda, ikafuatia zamu ya Makuhani na Uzao kutoa matunda. Muziki ukapigwa kusindikiza utoaji matunda๐
----------------------------------------------------------- |
Baba Halisi akifanya shukurani ya kubariki matunda.
Makuhani wanaohudumu katika chumba cha fedha wakipokea shukrani ya kubarikiwa kutoka kwa Baba Halisi
Uzao wakipokea Baraka ya Shukurani kutoka kwa Baba Halisi. Kulia ni Mama Halisi. Baba Halisi akimtia kichwani Maji ya Baraka (Damu Safi Nyeupe) kumbariki mmoja wa Makuhani anayehudumu katika Chumba cha Fedha, kufuatia kuvuliwa Moyo wa zamani. Baba Halisi akimtia kichwani Maji ya Baraka (Damu Safi Nyeupe) kumbariki mmoja wa Makuhani anayehudumu katika Chumba cha Fedha, kufuatia kuvuliwa Moyo wa zamani. Baba Halisi akimnywesha Maji ya Baraka (Damu Safi Nyeupe) kumbariki mmoja wa Makuhani anayehudumu katika Chumba cha Fedha, kufuatia kuvuliwa Moyo wa zamani. Baba Halisi akimnywesha Maji ya Baraka (Damu Safi Nyeupe) kumbariki mmoja wa Makuhani anayehudumu katika Chumba cha Fedha, kufuatia kuvuliwa Moyo wa zamani. Baba Halisi akimtia Maji ya Baraka (Damu Safi Nyeupe) kumbariki mtoto wa mmoja wa Makuhani anayehudumu katika Chumba cha Fedha, kufuatia kuvuliwa Moyo wa zamani.
------------------------------------------------------- |
Baadhi ya Makuhani na uzao wakiwa kwenye Ibada hiyo.
Makuhani na Uzao wakiwa kwenye Ibada hiyo.
Wasaidizi Baba na Mama Halisi wakipokea Baraka kutoka kwa Baba Halisi wakati wa somo la Kuvuliwa moyo wa zamani. Kulia ni Kaka Huduma. Baba Halisi akimnywesha Maji ya Baraka (Damu Safi Nyeupe) Kaka Huduma Mpya.
Baba Halisi akimtia Maji ya Baraka (Damu safi Nyeupe) mmoja wa Wasaidizi hao kumpariki. Kisha Ukafika Muda wa Baba Halisi kuhamasisha Makuhani na Uzao kuwa tayari kushiriki kwa hali na mali kufanikisha safari ya Hija ya Kigoma๐
Baba Halisi akionyesha mabango ambayo yatawekwa maeneo mbalimbali mkoani Kigoma, kuwandaa watu kuhudhuria Ibada kubwa ya Hija ya Chanzo Halisi itakayo fanyika mkoani humo tarehe 27 mwezi huu (26 Thebeti Majira Halisi), Mabango hayo yatawekwa maeneo mbalimbali ikiwemo Ujiji, Mwanga Centre, Bigabiro, Stendi Kuu ya Mabasi Kigoma Mjini na Uwanja wa Lake Tanganyika ambako Ibada Kuu ya Hija hiyo itafanyika. Baba Halisi akiendelea kueleza kuhusu mabango hayo
Kisha Baba Halisi akahamasisha Makuhani wajitokeze kujitolea kuchangisha uchapaji wa mabango makubwa zaidi ya aina hiyo yatakayokuwa Kigoma.
"Haya mabango tutayachapisha makubwa kuliko haya yaliyopo hapa, sasa nataka Makutani watano waje hapa ili kila mmoja achague bango atakaloshughulikia", akasema Baba Halisi. Na Baada ya kusema hivyo makuhani zaidi ya watano wakajitokeza hara๐
๐Baada ya kujitokeza makuhani hao wakaanza kila mmoja kuchagua bango la kushughulikia, huku Baba Halisi akiwatazama wakati wakiorodheshwa na Kuhani Faida๐.
--------------------------------------------- |
Baba Halisi akiwaombea Baraka Makuhani na uzao hao.
Baadhi ya Uzao na Makuhani wakitoa michango yao ya nauli zao za kwenda Hija hiyo.
Mama Halisi akimhudumia Maji (Damu Safi Nyeupe) Baba Halisi mwishoni mwa Ibada hiyo. Kushoto ni Kaka Halisi.
©2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo
Post a Comment