Mangula akipanda mti wa kumbukumbu
Na Hamida Ramadhani Dodoma
MAKAMU mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Tanzania bara, Philip Mangula amewataka viongozi na wanachama chama hicho kuwa na utaratibu wa kukutana katika vikao mara kwa mara kwani uimara wa chama ni mikutano.
Mangula ameyasema hayo leo Wilayani Kondoa katika Kijiji cha Bumbuta kwenye shetehe za maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa cha Mapinduzi (CCM ).
Makamu huyo amesema wanachama na viongozi wakikutana na kuongea mara kwa mara ndiko kutasaidia kukijenga chama cha Mapinduzi CCM.
" Muwe na utaratibu wa kukutana kila Mwezi na kuzungumza kwani kuna kero na mambo mengi ya kuonge yanayohusu chama chetu cha Mapinduzi CCM na jambo kubwa niwasisitize mnapakutana usidharau jambo la mtu mtu akileta jambo lichulie na kama kiongozi lifanyie kazi,"Amesema Mangula
Sambamba na hilo amewataka wanachama hao wa CCM kudumisha utulivu na amani ya nchi kwani bila amani Taifa haliwezi kufanya kitu wala maendeleo yoyote.
" Hivi karibuni tumesikia mauaji yakitokea katika mikoa yetu sasa kama viongozi wa Chamamkae na mkutane kwenye vikao na kutolea ufafanuzi mambo haya ya mauaji kwa maslahi ya Chama na Taiga kwa ujumla
Kwa upande wake Pili Mbaga Karibu Wa chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Dodoma amesema ni kweli mkoa wa Dodoma kumezuka mauji ya wanawake wawili na wengine kijiji cha Zanka watano wa famili moja chazo kikohusishwa ni wivu wa mapenzi na kulipizana visasi huku akikisitiza wananchi kitoa taarifa kwa wageni wanaowatilia mashaka.
Naye Mbunge wa Jimbo Kondoa na waziri wa uwekezaji viwanda na biashara Ashatu Kijaji amesema wanajivunia mafanikio ya chama hicho yaliyopatikana katika miaka 45.
Amesema mwaka 1977 wakati chama hicho kinazaliwa jimbo la Kondoa vijijini haikuwa na shule ya sekondari hata moja wala kituo cha afya.
Alisema hadi sasa jimbo jilo lina shule za sekondari 26 na vituo vya afya saba na tayari serikali imeshatoa fedha sh.milion 600 kwajili yakuomgeza kituo cha afya kingine katika kata ya KK.
"Tunaposherekea miaka 45 ya CCM sisi kama wana kondoa tunajivunia uboreshwaji wa huduma za jamii ikowemo huduma ya afya,maji,miundombinu ya barabara na umeme,"alisema
Post a Comment