Na CCM Blog, Mwanza
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel, amesema Serikali inathamini nafasi ya Redio katika kusaidia maendeleo ya Mkoa na nchi ya Tanzania kwa ujumla na kwamba wakati wowote ule Waandishi wa Habari za Redio wanayo fursa ya kukutana naye ofisini kwa ajili ya kuhabarisha na kuibua hoja za kimaendeleo mkoani Mwanza.
Amesema hayo leo katika Kongamano la Waandishi wa Habari, Mameneja wa Redio na Wahariri toka Redio mbalimbali mkoani hapo, ikiwa ni katika kuadhimisha Siku ya Redio Duniani 2022, ambayo kilele chake hufanyika Februari 13, kila mwaka.
Kongamano hilo limeratibiwa na Shirika la Internews, kwa kushirikiana na FHi360, na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC) ambayo iko chini ya Muungano wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).
Kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Habari kwa mwaka huu 2022 ni "Redio na Uaminifu" ambayo inasisitiza mambo makuu matatu; "Waandishi wa Redio kuwa wabunifu na waadilifu", "kuwajua wasikilizaji na kuwapatia maudhui yanayolingana na mahitaji" na "Redio kutengeneza vyanzo vya fedha ili kukabiliana na masuala ya kiuchumi".
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel
Post a Comment