Featured

    Featured Posts

RAIS DK. MWINYI AOMBOLEZA KIFO CHA MTOTO WA MZEE MALECELA, DK. MWELE MALECHELA

Na CCM Blog

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee John Malecela kufuatia kifo cha mwane Dk. Mwele Ntuli Malecela aliyefariki Juzi, Februari 10, 2022, jioni mjini Geneva, Uswisi wakati akipatiwa matibabu.

Ikulu ya Zanzibar imesema Rais Dk. Mwinyi pia ametoa salamu hizo za pole kwa ndugu jamaa na marafiki pamoja na uongozi wote wa Shirika la Afya Duniani (WHO), ambapo hadi Dk, Mwele umauti unamfika alikuwa ni Mkurugenzi wa Udhibiti wa Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele.

Katika salamu hizo za rambirambi, Rais Dk. Mwinyi ameeleza kusikitishwa kwake na kifo hicho na kuwasihi ndugu, jamaa na marafiki pamoja na uongozi wote wa WHO kuwa na subira na ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo.

Rais Dk. Mwinyi amemuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Dk. Mwele mahala pema peponi.

Dk. Mwele aliyezaliwa Machi 26, 1963, katika uhai wake aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za kiafya Tanzania (NIMRI) ambapo pia, aliwahi kuwania nafasi ya mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi.
Marehemu Dk. Mwele enzi za uhai wake.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana