Hiyo ni sehemu ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za serikali CAG iliyowasiliahwa Jumatano Ikulu. Jijini Dodoma, leo.
Akiwasilisha ripoti ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2021 kwa Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu Chamwino Kichere ripoti imebaini kasoro na imetoa ushauri nini kifanyike kulingana yale iliyoyabaini katika ukaguzi.
Amesema katika mwaka 2020/21 amefanya kaguzi maalumu 56, kaguzi 37 zikiwa za mamlaka za Serikali za Mitaa, 12 Serikali kuu na sita mashirika ya umma na moja ya mifumo ya Tehama.
“Katika mwaka 2020/21 nimetoa jumla ya hati 999 za ukaguzi, kati ya hizo, hati 185 za mamlaka za Serikali za Mitaa, 195 mashirika ya umma, hati 308 serikali kuu, hati 19 vyama vya siasa, hati 292 miradi ya maendeleo,” amesema.
Amesema kati ya hati 999 nilizotoa, hati zinazoridhisha ni 970, sawa na asilimia 97.1, hati zenye mashaka ni 19, sawa na asilimia 1.9, hati mbaya ni sita na nilitoa hati 4 za kushindwa kutoa maoni.
Amesema hati mbaya na mashaka zimepungua katika ukaguzi huo ikilinganishwa na mwaka jana.
Kichere amesema kuna ongezeko la hati safi kutoka asilimia 89 kwa mwaka jana hadi asilimia 98.01 mwaka 2020/2021.
Amezitaja taasisi zilizopata hati zenye mashaka kuwa ni Jiji la zamani la Dar es Salaam, Halmashauri za Wilaya ya Kisarawe (Pwani), Longido (Arusha), Mlele (Rukwa), Musoma (Mara), Sengerema (Mwanza) na Bunda (Mara).
Kichere amesema kwa upande wa mashirika ya umma, taasisi zilizopata hati yenye mashaka ni Mamlaka ya Maji na Ustawi wa Mazingira Geita, Muleba, Ngara (Kagera), Tabora, Taasisi ya Mifupa Muhimbili na Mamlaka ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).
Post a Comment