Na Mwandishi Maalum
Nyota wa muziki wa kizazi kipya, Gift Stanford, ‘Gigy Money’ amewataka wazazi na walenzi nchini kuwapa fursa watoto ya kuonyesha vipawa walivyo navyo kwani katika dunia ya sasa vipaji ni fursa muhimu.
Staa huyo aliyasema hayo, Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo , wakati wa hafla ya Usiku wa Wanawake wa Mkongo, iliyokuwa imeandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika kata hiyo kwaajili ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan na kuhitimisha Siku ya Wanawake Duniani.
Akichangia mada, Gigy Money, amesema ametokea katika familia duni na mama yake hakuamini kama anakipaji cha uimbaji badala yake aliamini kujihusisha na muziki basi angekuwa mhuni.
“ Nilikuwa na kipaji lakini mama yangu alikuwa hajawahi kukiona. Watoto wengi tuna vipaji lakini tunaogopa kuvionyesha tukiamini wazazi wetu wataona ni uhuni au tumeharibikiwa,”ameeleza nyota huyo.
Amesema kabla ya kujikita zaidi katika muziki aliamua kumhakikishia mama yake kwa kumtunza na kumjali ili aamini kipaji.
Gigy ameeleza yeye ni mama wa mtoto mmoja aitwaye Mayla ambaye ana mlea mwenyewe.
“Mama yangu alinilielea akiwa peke yake. Alinionyesha wanamke tuna nguvu zaidi ya mwanaume.Sisi ni chanzo cha dunia,”ameeleza.
Aliongeza; “Sitamani kuona mwanamke yoyote ana mtoto anayetamani kuimba amzuie. Hujui atakuwa nani. Hujui atakuja kukusaidia vipi kupitia kipaji chake,” alieleza staa huyo anayetamba na nyimbo zake za Papa, Sasambu, Njoo, Ok na Shoga.
Mwenyekiti wa UWT, Kata ya Maokongo, Abbriaty Kivea, amempongeza Rais Samia kwa uwajibikaji na kupambania haki za wanawake huku akiwataka watanzania kuunga mkono. Pia amewataka wanawake kujiamini na kujua haki zao katika ndoa.
Abbriaty ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alisema wanawake wengi wana poteza haki zao katika ndoa kutokana na kuto kuzijua haki zao ama kujiona wanyonge mbele ya wanaume jambo linalowafanya kudhurumiwa.
“Kuna wanawake wengi tunaishi na wanaume katika ndoa lakini unapofikia wakati wa kuachana wengi hawajui haki zao”ameeleza Abrriaty.
Nyota wa muziki wa kizazi kipya Gift Stanford, ‘Gigy Money’ (kushoto) akitumbuiza katika hafla ya Usiku wa Wanawake wa Kata ya Makongo, iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa kata hiyo, Kinondoni, Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. Kulia ni Mwenyekiti wa umoja huo wa kata hiyo, Abbriaty Kivea. (Picha Mpigapicha Maalum).
Post a Comment