Muswada wake huo sasa umepelekwa kwa kamati ya Bunge la Marekani inayoshughulika na masuala ya mambo ya nje.
Vikwazo vilivyopendekezwa vinajumuisha kuzuia misaada kutoka nje, kusitisha uuzaji wa ndani na nje wa silaha, udhibiti katika vikwazo vya bidhaa na vikwazo vingine vya kifedha.
Huku wengine wakitaka kutolewa kwa adhabu kwa mtu au nchi zinazofanya biashara na nchi iliyotangazwa na kudaiwa kuwa mfadhili wa ugaidi.
Mbali na Pakistani nchi nyingine zinazodaiwa kuwa wafadhili wa ugaidi ni Cuba, Korea Kaskazini, Iran na Syria.
Machi 9, 2022 wabunge Scott Perry, Gregory Steube na Mary E. Miller walituma barua kwa Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Merrick Garland wakidai kuwa na wasiwasi juu ya uhusiano wa karibu wa Balozi Masood Khan na watendaji wa ndani wanaohusishwa na utawala wa Pakistani.
Wabunge hao watatu wa Marekani wametaka uchunguzi ufanyike kuhusu madai ya Khan ambaye tayari amethibitishwa kuwa Balozi wa Pakistan nchini Marekani, kuwa na uhusiano na makundi ya ugaidi.
Mwezi uliopita, mbunge mwingine wa Marekani alijaribu kutaka kufanya maandamano kuzuia ubalozi wa Khan nchini humo, lakini utawala wa Rais Joe Biden ulikataa maandamano yake na kuthibitisha uteuzi huo.
Masood Khan, balozi mpya wa Pakistan nchini Marekani ni mwanadiplomasia mkuu ambaye aliwahi kuwa mwakilishi wa kudumu wa Islamabad katika Umoja wa Mataifa mjini New York, Pia alikuwa rais wa Azad Kashmir hadi Agosti mwaka 2021.
Post a Comment