Magazeti ya leo, gazeti la mwananchi, global publisher, habari leo, habari mpya, ippmedia,magazeti ya leo tanzania, magazeti ya udaku, michuzi, michuzi blog, mpekuzi huru, mwananchi, mwanaspoti,nipashe, sekretarieti ya ajira
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama ameelezea mafanikio lukuki yaliyopatikana katika mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ambapo ameitaja moja ya taasisi zilizo chini ya wizara hiyo, Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kuwa miongoni mwa zilizofanikisha mafanikio hayo. Waziri Mhagama ameitaja MKURABITA alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kuhusu mafanikio hayo jijini Dodoma Machi 16, 2022.
Waziri Mhagama akibadilishana mawazo na Mratibu wa MKURABIRA, Dkt. Seraphia Mgembe alipoitembelea taasisi hiyo Machi 15, 2022, Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya MKURABITA baada ya kumaliza kikao nao Makao Makuu ya Taasisi hiyo eneo la Nane Nane, Nzuguni jijini Dodoma.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Waziri Mhagama akiitaja MKURABITA kuwa moja ya taasisi zilizofanikisha mafanikio hayo baada kuwezeshwa na Serikali zaidi ya sh. blioni 3..
Post a Comment