Featured

    Featured Posts

WAZIRI MKENDA ASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA KUJADILI MABADILIKO CHANYA KATIKA MAENDELEO


Prof Adolf Mkenda Waziri wa Elimu Sayansi an Teknolojia akiwa katika Picha na Baadhi ya Mawaziri waluohudhururia Jukwaa la majadiliano ya kuleta mabadiliko sahihi katika Elimu ylililofanyika sambamba na Mkutano wa Kimataifa wa Maendeleo Doha Forum,jijini Doha, Qatar
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Viongozi kutoka UNICEF walipokutana katika Mkutano wa Kimataifa wa Maendeleo DOHA FORUM  unaofanyika Jijini Doha, Qatar.

 Prof Adolf Mkenda Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia akiwa katika mazungumzo maalum na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Education Above All la Qatar Fahad  Al- Sulaiti juu ya ushirikiano na Tanzania katika kuimarisha elimu Doha Qatar


Na.WyEST



Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda   ameshiriki Mkutano wa Kimataifa  Doha Forum kuhusu masuala ya Maendeleo uliofanyika Machi 26 ,2022.


Mkutano huo unaofanyika  kila Mwaka  umeshirikisha viongozi na wataalamu kutoka nchi mbalimbali Duniani ambapo Mwaka huu umelenga katika kujadili jinsi ya kuleta mabadiliko chanya katika maendeleo.


Moja ya Agenda katika mjadala wa mkutano huo ni mabadiliko halisi na chanya  katika elimu hususa baada ya athari za UVIKO 19 ambapo Waziri wa Elimu ameshiriki katika majadiliano hayo ambayo yanahusisha Mawaziri kutoka Nchi 9 ikiwemo Qatar ,Tanzania,Uganda, Sudan Kusini, Siera Leone na Somalia.


Akizungumza katika jukwaa hilo la majadiliano  Prof. Mkenda amesema Tanzania kwa sasa iko katika hatua ya kufanya mapitio ya Sera na Mitala ili kuhakikisha Elimu inayotolewa inazingatia kujenga ujuzi na kwamba mpango huo ni shirikishi.


Nae Mtendaji Mkuu wa Shirika la Education Above all la Qatar Mhe. Fahad Al-Sulaiti  amesema wakati umefika wa mataifa kuleta Mabadiliko sahihi katika Elimu kwa kuwa na Mitaala Sahihi, mbinu za kisasa za kufundishia, matumuzi ya TEHAMA katika kufundisha na ujifunzaji kulingana na mipango endelevu ya Nchi na kusisitiza juu ya suala la kuongeza uwekezaji katika Sekta ya Elimu.


Wakati huo huo Waziri wa Elimu amekutana na kufanya  mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji huyo juu ya ushirikiano katika kuboresha Elimu Tanzania.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana