Featured

    Featured Posts

DC IKUNGI : TANZANAIA BARA HAIWEZI KUWA SALAMA KAMA ZANZIBAR HAITAKUWA SALAMA, KIUCHUMI, KIJAMII.

Ikungi, Singida
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Jerry Murro amesema Tanzania Bara haiwezi kuwa salama kama Zanzibar haitakuwa salama kiulinzi, kiuchumi na kijamii.

Amesema wakati dunia ikiungana katika muktadha mbalimbali ni vizuri kwa Tanzania kudumisha Muungano wao ili kutoa nguvu ya kuleta maendeleo kwa jamii za pande zote mbili za Muungano huo.

Muro ameyasema hayo wakati akifungua Kongamano la Vijana mkoa wa Singida, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar  ambapo alifungua kongamano hilo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo Dk. Binilith Mahenge.

Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa mikutano ya chuo cha uhasibu Singida ambapo mada mbalimbali zimejadiliwa ikiwemo umuhimu wa kudumisha muungano, fursa za uchumi katika mkoa wa singida na ushiriki wa vijana katika sensa ya watu na makazi.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Jerry Murro akizungumza katika Kongamano hilo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana