Moshi, Kilimanjaro
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)-Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amesema ziara ambayo Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea nayo Nchini Marekani, ni muhimu kwa kuwa ina tija kubwa Kiuchumi.
Amesema ziara hiyo ya Marekani ina tija ana manufaa makubwa kiuchumi kwa imemkutanisha na viongozi wakubwa akiwemo Makamu wa Rais wa nchi hiyo Kamala Harris, ambaye nchi yake ina ushawishi mkubwa duniani.
Pia amempongeza Rais Samia kwa kufanya kazi kwa bidii kubwa ya kuwaletea Watanzania maendeleo katika kupindi cha mwaka mmoja tu alichokaa madarakani.
Kinana ameyasema hayo leo mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro alipokuwa akizungumza na Wanachama wa CCM wa mkoa huo akiwa katika siku ya tangu ya ziara yake ya kwanza mikoani, kukagua na kujenga uhai wa Chama na kujitambulisha tangu alipochaguliwa Aprili Mosi Mwaka huu, jijini Dodoma.
Ziara hiyo ya kukagua na kujenga uhai wa Chama na kujitambulisha tangu alipochaguliwa Aprili Mosi Mwaka huu, jijini Dodoma, Kinana aliianza juzi, katika mkoa wa Pwani na jana akawa mkoani Tanga ambapo baada ya mkoa wa Kilimanjaro kesho anatarajiwa kwenda mkoani Arusha.
"Sasa hivi Rais anafanya ziara huko nje kwa wafadhili, watoa mikopo, ili tuweze kupata fedha nyingi zaidi kwa maendeleo ya taifa letu, huko Marekani, ameonana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais waMrekani.
Marekani ni nchi kubwa, Marekani ina kauli duniani, Marekani ni mshiriki wetu wa maendeleo katika sekta mbalimbali zinazowagusa wananchi," Kinana akasema kwa msisitizo.
Kinana amesema Rais Samia huko Marekani, mbali na mbali na kukutana na kuzungumza na Makamu wa Rais wa nchi hiyo, pia amekukutana na kuzungumza na viongozi wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha duniani (IMF), Taasisi ambazo ni washirika muhimu wa maendeleo na uchumi wa Tanzania, hivyo Rais anastahili pongezi.
Post a Comment