Featured

    Featured Posts

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM KANALI MSTAAFU ABDULRAHMAN KINANA , APIGA KURA KUCHAGUA VIONGOZI WA SHINA NO 9, TAWI LA MASAKI, KATA YA MSASANI MKOANI DAR ES SALAAM.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana leo Aprili 19 , 2022 ameungana na Wanachama wenzake wa Shina Namba 9, Tawi la Masaki, Kata ya Msasani wilaya ya Kinondoni, Mkoani Dar es Salaam kufanya uchaguzi wa Viongozi katika Shina lao. Nafasi zilizopigiwa Kura ni Mwenyekiti wa Shina na wajumbe wanne wa Kamati ya Shina.

Katika uchaguzi huo, Ndg Kizito Mahamba aliibuka kidedea baada ya kupata kura 108 za ndiyo kati ya kura 109 zilizopigwa huku moja ikiwa ya hapana.


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana leo Aprili 19 , 2022 akisalimia Wanachama  wenzake wa Shina Namba 9, Tawi la Masaki, Kata ya Msasani wilaya ya Kinondoni, Mkoani Dar es Salaam wakati akiwasili katika  uchaguzi wa Viongozi Shina namba 9  katika nafasi ya Mwenyekiti wa Shina na wajumbe wanne wa Kamati ya Shina.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana leo Aprili 19 , 2022 akizungumza na kufurahi Pamoja na Mwanachama Mwenzake wa Shina Namba 9 Bibi Christina Kilindo katika  uchaguzi wa Viongozi Shina hilo  katika nafasi ya Mwenyekiti wa Shina na wajumbe wanne wa Kamati ya Shina.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana  akiwa Katika Mkutano Mkuu wa Shina Namba 9 leo Aprili 19 , 2022
Mwanachama wa Shina Namba 9 akipiga kura ya Kuchagua Viongozi wa Shina hilo ,Nyuma pichani ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akiwa katika mstari wa kupigia kura leo Aprili 19 , 2022

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana leo Aprili 19 , 2022 akiweka Karatasi ya kura katika boksi maalum la kupigia kura ya kumchagua Mwenyekiti wa Shina Namba 9 Tawi la Masaki, Kata ya Msasani wilaya ya Kinondoni, Mkoani Dar es Salaam.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana wakifurahia Matokeo ya Uchaguzi pamoja na  Wanachama  wenzake wa Shina Namba 9, Tawi la Masaki, Kata ya Msasani wilaya ya Kinondoni, Mkoani Dar es Salaam.
Mshindi wa Kiti Cha Uenyekiti wa Shina Hilo Ndugu, Kizito Mahamba alieibuka kidedea baada ya kupata kura 108 akizungumza na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Tawi hilo.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana