Featured

    Featured Posts

KINANA AUNGANA NA WANACHAMA WENZAKE KUCHAGUA VIONGOZI WA SHINA LAO LA CCM, LEO.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akipiga kura kumchagua Mwenyekiti wa CCM Shina la Namba 9, Tawi la Masaki, Kata ya Msasani Jijini Dar es Salaam, katika Uchaguzi uliofanyika leo kwenye Shina hilo.

Katika Uchaguzi huo nafasi zilizopigiwa kura zilikuwa ni Mwenyekiti wa Shina na Wajumbe wanne wa Kamati ya Shina ambapo Mwanachama wa shina hilo Ndugu Kizito Mahamba alishinda na kutangazwa mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti kwa kujipatia kura 108 za ndiyo na moja ya hapana kati ya kura 109 zilizopigwa.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akisalimia wanachama wenzake wa shina namba 9, Tawi la Masaki, Kata ya Msasani, Jijini Dar es Salaam, alipowasili kushiriki katika Uchaguzi huo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akisalimia wanachama wenzake wa shina namba 9, Tawi la Masaki, Kata ya Msasani, Jijini Dar es Salaam, alipowasili kushiriki katika Uchaguzi huo.
Aliyekuwa mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti wa Shina namba 9, Ndugu Kizito Mahamba akizungumza baada ya kushinda katika Uchaguzi huo
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana na wanachma wenzake wa CCM Shina namba 9, Tawi la Masaki, wakifurahi baada ya matokeo ya uchaguzi huo kutangazwa.
"Nimefurahishwa sana kwa uchaguzi huu kumefanyika kwa Demorasia ya hali ta juu", pengine ndivyo Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Ndugu Kinana alivyokuwa akimwambia mwanachama mwenzake huku wakitabasamu, baada ya matokeo kutangazwa katika uchaguzi huo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana