Na Mwamvua Mwinyi,Kibiti
MKE wa Rais Mstaafu awamu ya nne, Salma Rashid Kikwete (MB)Jimbo la Mchinga mkoa wa Lindi, ametoa Rai kwa Watanzania kuendelea kulinda Tunu ya Muungano na amani iliyodumu tangu enzi ya waasisi wetu akiwemo mwl.Julius Nyerere ,kwa maslahi ya vizazi vijavyo.
Aidha amefafanua, maadili yanaporomoka ,na hii Ni kutokana na kukosa elimu ya dini na kutozingatia misingi ya kidini na kusisitiza kupeleka watoto kupata elimu ya dunia na Akhera,Quran kwa maendeleo Yao baadae.
Akizungumza katika Kongamano la Dua ya siku mbili ,la wanawake wa Kiislamu (JUWAKITA BAKWATA) Mkoani Pwani,Kumuombea Dua’a Njema ,Rais Samia Suluhu Hassan ,lililofanyika wilayani Kibiti ,alieleza bila amani hakuna maendeleo,;”: amemuomba Allah ashushe neema zake katika amani na Muungano uliodumu nchini na kuondosha tofauti zilizopo baina ya baadhi ya mataifa ulimwenguni.
Alisema wakati akiombewa Rais Samia pia aombewe Rais wa Zanzibar dkt.Hussein Mwinyi kwa kushirikiana nae kufanya kazi nzuri na ,kupambana kutatua changamoto mbalimbali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Binadamu tunaishi kwa Dua ,kila Jambo ,kila mmoja wetu Ni shahidi wa kuona namna gani Rais Samia anavyotupambania Watanzania”na kuhangaikia tunachokitaka nchini ili kuinua Uchumi wa Taifa letu” ‘:;”,Tumshukuru mungu kulinda Muungano wa kuigwa Afrika na mataifa yote , kwenye awamu zote zilizopita tangu kwa waasisi wetu tangu enzi ya mwl.Julius Nyerere.”
“Hakuna pengine tunu ya Muungano iliyoendelezwa,tumelinda Muungano ambao umeleta amani na upendo ,tuombee tunu hii kwa maslahi ya vizazi vijavyo na udumu Karne na Karne na kutukuza busara za waasisi hao “alibainisha Salma.
Katika hatua nyingine, alisema Dunia inatambua mama Shupavu Rais Samia Suluhu Hassan,Na hii yote Ni kwa ajili ya kupata elimu bora.
Salma aliwasihi wanawake na jamii kupeleka watoto shule kupata elimu dunia na elimu akhera ,”Quran.
“Wakati ni huu tusome,Jambo jingine maadili,kadri tunavyozungumza yanaporomoka,na hii kwasababu hatusomi dini “alieleza.
Aliwaasa Watanzania kujitokeza katika Zoezi la Sensa 23 agost mwaka huu kwa Ajili ya kupata takwimu sahihi ya watu na kusaidia mipango mizuri kwa maendeleo ya nchi.
Aliwapongeza JUWAKITA Pwani, kufanya Jambo kubwa ,jema kwenye Uislam,na kusema na hayo ndio mambo yanatakiwa kufanywa na viongozi wa dini ,mojawapo kukutanisha waumini wa kiislam
Kwa upande wake ,Naibu Waziri wa Maendeleo ya jamii, Wanawake,Jinsia na Makundi maalum,Mwanaidi Hamis alieleza , nao Kama Wizara wameungana na wanawake hao kwa kuliombea Dua Taifa na Serikali.
Alisema Dua hii itampa Rais Imani,ujasiri katika kutekeleza majukumu yake katika kutatua kero mbalimbali kwenye jamii zetu.
“Nawataka wanawake tuwe majasiri ,na tuwe wawazi kwa Yale yanayotukuta katika jamii, ili kupata haki kwani uwazi Ni ushindi ,:”;Tusifiche yanayotukumba kimbilieni fursa zilizopo katika Serikali hii”Rais wetu anaumia kusikia mwanamke kapigwa ,ananyimwa haki ,hivyo Basi tufunguke kutetea haki zetu”alisisitiza Mwanaidi.
Akiongea kwa njia ya simu Waziri wa wanawake,jinsia , watoto na wazee Zanzibar alisema,Rais anafanya kazi kubwa,na kuunda Wizara hiyo ambapo upande wa Zanzibar kuhakikisha kundi la wanawake linapiga hatua kimaendeleo.
Alimshukuru Rais kwa kuendelea kuliongoza Taifa kwa utulivu na kuinua uchumi na maendeleo kwa Kasi .
Mwenyekiti JUWAKITA BAKWATA Pwani ,Shukuru Ngoma alisema Lengo la mkusanyiko huo ambao umeungwa mkono pia na wengine waliotoka mikoa jirani Ni kumuombea Dua kwa kuhakikisha nchi ipo imara,amani na kufanya makubwa katika mwaka mmoja tangu awe Rais.
Alieleza ,mwezi huu wa Ramadhan Ni wa kheri toka kwa Allah ambapo nao wamekesha ili Allah aendelee kumsimamia katika kazi zake .
Shukuru aliomba kudumishwa amani , utulivu na upendo katika Taifa .
Nae Shamim Khan ambae ni Mwenyekiti wa JUWAKITA Taifa, alimshukuru mh.mufti kuunganisha waislam bila ubaguzi ikiwemo kutobagua usawa wa uongozi kijinsia.
Alimpongeza Rais kwa kazi zinazoendelea kufanywa katika sekta ya afya,elimu, miundombinu na sekta nyingine na aliwataka watendaji wa chini kwenda na kasi iliyopo.
Alishauri jamii isipuuze Kuwa Covid 19 imekwisha Bali watu waendelee kuchanja chanjo ya Covid 19 na kusisitiza wanawake kupeleka watoto wao kupata chanjo ya polio .
Akitoa salamu za mkoa Mkuu wa mkoa wa Pwani ,alhaj Abubakari Kunenge, alisema Dua Ni miongoni mwa ibada kwa mola .
Aliishukuru JUWAKITA kwa kutambua tunu tuliyopewa katika nchi yetu pamoja na kutambua kazi anazozifanya na kutatua kero za wananchi.
Kunenge alielezea kuwa ,Dua na visomo vilivyofanywa kwa hakika Allah atamlipa mja wake Rais Samia na atawalipa wote waliojitokeza kwa Dua hiyo.
Awali Zainab Vullu alisema Dua hiyo Ni thamani ya shukran kwa Rais Samia,kwani hakuna zaidi ya Dua , kwakuwa ni sadaka ili kumzawadia ikiwa ni shukran kwa anayoyafanya nchini na dua hiyo ikaendelea kumpa ulinzi.
Post a Comment