Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati akumuelezea kuhusu bidhaa mbalimbali za Kilimo kabla ya kuzindua na kugawa vitendea kazi kwa Maafisa Ugani wa Kilimo nchini katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia miche ya matunda ya miembe pamoja na michungwa katika mabanda ya Maonesho ya bidhaa za kilimo nje ya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali kabla ya kuzindua na kugawa vitendea kazi kwa maafisa Ugani wa Kilimo katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe,akizungumza wakati wa uzinduzi na ugawaji wa vitendea kazi kwa maafisa Ugani wa Kilimo katika hafla iliyofanyika leo April 4,2022 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela ,akizungumza wakati wa uzinduzi na ugawaji wa vitendea kazi kwa maafisa Ugani wa Kilimo katika hafla iliyofanyika leo April 4,2022 Jijini Dodoma.
SEHEMU ya Maafisa Ugani wa Kilimo wakifatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati wa kuzindua na kugawa vitendea kazi kwa maafisa Ugani wa Kilimo katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia aina mbalimbali ya zao la mpunga ambao umekobolewa katika viwango mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya binadamu na utengenezaji wa nafaka kwa ajili ya mifungo katika Maonesho yaliyofanyika nje ya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia mchele uliowekwa kwenye kifungashio kwa ajili ya kupelekwa sokoni katika Maonesho yaliyofanyika nje ya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022. Kushoto ni Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo la Taifa Jacqueline Mkindi kuhusu zao jipya la kilimo pamoja na mazao mbalimbali ya Biashara katika Maonesho yaliyofanyika nje ya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kuhusu zao la parachichi ambalo limekuwa likiwaletea tija wakulima nchini hususan katika Mikoa ya Njombe, Mbeya, Arusha na Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Kilimo Hussein Bashe mara baada ya ukaguzi wa mabanda mbalimbali ya wakulima pamoja na Wafanyabiashara leo tarehe 04 Aprili, 2022 Jijini Dodoma.
Wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa Kilimo wakiwa katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi na ugawaji wa vitendea kazi kwa Maafisa Ugani wa Kilimo nchini uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akigawa pikipiki kwa waakilishi wa Maafisa Ugani 7000 katika hafla iliyofanyika nje ya Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04, Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo wakati akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa pikipiki 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani Kilimo wa nchi nzima katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe wakati akielezea kuhusu vitendea kazi kwa Maafisa Ugani Kilimo kabla ya uzinduzi katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu akimkabidhi mfano wa Ufunguo wa Pikipiki Waziri wa Kilimo Hussein Bashe mara baada ya kuzindua ugawaji wa pikipiki hizo 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu akiwasha Pikipiki mara baada ya kuzindua ugawaji wa pikipiki hizo 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka mara baada ya kuzindua ugawaji wa pikipiki hizo 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani nchini katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.
…………………………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
Kwa upande wake Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezipongeza taasisi za fedha kwa kuwapatia mitaji wakulima kwa viwango vya kuridhisha ambapo kila mkulima anaweza kumudu
‘Nalipongeza bunge kupitia kamati ya kilimo, mifugo na maji kwa kazi nzuri ya kushauri na kuisimamia serikali kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi lakini pia kupitisha bajeti kwaajili ya utekelezaji wa miradi yote ya kilimo.’amesema Mhe Majaliwa
Naye Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amemuomba Rais Samia kumpatia Sh150 bilioni ili aziweke katika benki za biashara kama dhamana (security), hatua itakayowezesha wakulima nchini kuanza kupata ruzuku ya mbolea katika msimu wa kilimo ujao.
Amesema Rais Samia aliielekeza Benki Kuu (BoT) kutenga Sh1 trilioni kwa ajili ya sekta ya kilimo na kumuomba Sh150 bilioni kwa ajili ya kuweka katika benki za biashara kama security.
Amesema hatua hiyo itawezesha kuaanza kutoa ruzuku ya mbolea katika msimu ujao wa kilimo.
Aidha Bashe alisema,licha ya mipango na mikakati mingi iliyopo lakini kumekuwa na changamoto kubwa ya pembejeo huku akisema kwa uoande wa mbolea katika soko la Dunia kwa sasa imepanda kwa zaidi ya asilimia 300.
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa amesema kuwa ofisi yake wamefanya vikao na wataalam wao na watatekeleza maagizo yote kutoka kwa wizara ya kilimo na hakutakuwa na visingizio baada ya kuwapatia vitendea kazi kupatikana.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amesema kuwa Mkoa waliweka nguvu kubwa katika kilimo Cha Alizeti ambapo Kwa takwimu zilizopo wameweza kufanya vizuri.
“Sisi kama Dodoma tulikubaliana kuweka nguvu kwenye kilimo Cha Alizeti na tumefanya vizuri tunashirikisha watu wa mabenki ili kufanya kilimo chenye tija tumshukukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi Dodoma”amesma Mtaka
Post a Comment