Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tamzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Tuzo Maalumu kwa mchango wake wa kuthamini na kusimamia vema Sekta ya Sanaa nchini.
Tuzo hiyo imetolewa na Shirikisho la Muziki Tanzania Aprili 02, 2022 jijini Dar es Salaam wakati wa utoaji wa Tuzo za Muziki nchini za mwaka 2021 na kupokelewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa niaba ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Miongoni mwa kazi kubwa zilizofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita ni kufufuliwa kwa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa ambao lengo lake ni kuwakopesha wasanii na kuwapa mafunzo ili waweze kutoa kazi bora za Sanaa ambazo zitakuwa na ushindani ndani na nje ya Tanzania ambazo zitawafanya wasanii waweze kunufaika kwa kazi zao.
Aidha, katika Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita imeshuhudiwa
Post a Comment