Featured

    Featured Posts

RAIS SAMIA AZINDUA KAMPUNI YA WILMAR KUUZA MCHELE WA TANZANIA ULAYA+video

Rais Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Kampuni ya Wilmar Tanzania Limited, Stella Urio (kulia) kuhusu jinsi mchele huo wanavyouandaa na kufungasha kwa ubora unaotakiwa alipotembelea banda la kampuni hiyo jijini Dodoma Aprili 4, 2022.


Rais Samia Suluhu Hassani amezindua uuzaji wa mchele nje ya nchi unaofungashwa na Kampuni ya Wilma ya hapa nchini. Hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika baada ya Rais kutembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho yaliyofanyika sambamba na hafla ya kukabidhi kwa maafisa Ugani pikipiki 6700 na vifaa vya kupimia afya ya udongo jijini Dodoma Aprili 4, 2022. Akizungumza katika maonesho hayo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Kampuni hiyo Stella Urio amesema kuwa mchele huo hununuliwa kwa wakulima katika mikoa ya Mbeya, Morogoro na Kanda ya Ziwa.

Stella Urio na Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni hiyo, James Alva wakionesha nyuso za furaha baada ya Rais Samia kuzindua uuzaji wa mchele wao nje ya nchi.

PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

 Mdau, nakuomba sikilize kupitia clip hii ya video, Rais Samia akitamka kuzindua uuzaji wa mchele huo Ughaibuni huku Stella Urio akielezea mikakati yao ya kupanua soko la mchele wao wenye chapa ya Korie....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
0754264203
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana