Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama amefungua mkutano wa pamoja na viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini jijini Dodoma Aprili 9, 2022 na kuwaeleza kuwa wanapaswa kupaza sauti kuishukuru Serikali inapotangaza ajira mpya za wafanyakzi kwani kwa upande wa vyama vinaongeza mapato na kuwa hai zaidi. Mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako (kulia) lengo lake lilikuwa ni kuelezea mtizamo wa Serikali ya Awamu ya Sita katika uimarishaji wa utumishi wa umma unaowajibika kwa hiari na matumizi ya mifumo ya Tehama katika utendaji na utoaji huduma bora katika utumishi wa umma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deo Ndejembi akimkaribisha Waziri Mhagama kufungua mkutano huo.
Viongozi wa vyama vya wafanyakazi wakifuatilia kwa makini wakati Waziri Mhagama akifungua mkutano huo.
Wanahabari wakisikiliza wakati Waziri Mhagama akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Waziri Mhagama na Waziri Ndalichako pamoja na Rais wa Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Nyamhokya wakizungumzia kuhusu mkutano huo.....
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
Post a Comment