Featured

    Featured Posts

MCHENGERWA AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUTEKELEZA AHADI


Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Rufiji.  Mhe,  Mohamed Mchengerwa amesema

Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetekeleza ahadi zote ilizotoa kwa  wananchi wa Rufiji na amewataka waendelee kushiriki kikamilifu kwenye masuala ya maendeleo ya kitaifa  ikiwa ni pamoja na  zoezi la Sensa    linalotarajiwa kufanyika Agosti 23, 2022 ilikuboresha maisha yao kwa ujumla.


Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo leo Mei 2, 2022  baada ya kukamilisha  zoezi la mbio   za Mwenge katika Wilaya ya Rufiji ambalo lilianza jana na kukagua miradi mbalimbali katika Wilaya hiyo.


Akimkaribisha Kiongozi wa mbio za Mwenge kwenye jimbo lake la Rufiji jana,  Mhe. Mchengerwa amesema tayari miradi yote iliyopangwa katika eneo hilo kulingana na bajeti imetekelezwa ambapo  hadi sasa utekelezaji wa miradi ya maendeleo umefikia asilimia 136.

"Ndugu Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2022, kwanza kabisa naomba nikukaribishe katika eneo letu la Rufiji, lakini pili nipende kumshukuru Rais wetu kwa kukamisha ahadi zote ilizotoa wakati wa uchaguzi". Amefafanua Mhe. Mchengerwa.


Pia ameishukuru Serikali kwa kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kilometa 37 ya  Nyamwage- Utete  kwa kiwango cha lami na Ikwiriri- Mkongo yenye kilometa 31.


Aidha ameongeza kuwa hadi sasa  Halmashauri ya Rufiji imebakiwa  na akiba ya zaidi ya 1.5 bilioni.


Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru wa  mwaka 2022, Sahili Nyanzabara  Geraruma  amempongeza Mhe. Mchengerwa kwa kuendelea kuwaletea makubwa wananchi wa Rufiji.

Akizungumza kwenye mradi wa uzinduzi wa ghala la kuhifadhia zaidi ya tani 300 katika eneo la mkombozi amesifu jitihada za Mhe. Mchengerwa za kushirikisha sekta binafsi kuwekeza katika miradi ambayo inawasaidia wananchi.


Geraruma  amezitaja salamu za mbio wa Mwenge wa mwaka huu kuwa ni pamoja na  wananchi kushiriki kikamilifu zoezi la Sensa  linasaidia pamoja na mambo mengine uundaji wa Sera na Mipango ya Serikali.


Salamu nyingine ni kupima virusi vya UKIMWI, kujikinga na malaria, kuepuka madawa ya kulevya na rushwa pamoja na kuzingatia lishe bora ili kuepukana na udumavu.


Mhe. Mchengerwa pia  ameshiriki kwenye risala ya utii kwa Mhe. Rais  wakati wa mbio hizo za Mwenge wa Uhuru.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana