Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, hafla itakayofanyika mkoani Arusha.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema uamuzi wa Rais kushiriki kwenye shughuli hiyo ni heshima kubwa kwa waandishi wa habari ikizingatiwa ratiba zake nyingi na siku hiyo kuwa sikukuu.
Waziri Nape amesema jambo hilo litaweka historia kwa Rais Samia kuwa Rais wa kwanza kuhudhuria hafla hiyo, na kwamba ni tafsiri ya kiu yake ya kuona sekta ya habari ikikua nchini.
Kila mwaka Mei 3 ni Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambapo mwaka 2022 Tanzania imepata fursa ya kipekee ya kuwa mwenyeji wa mkutano katika bara la Afrika.
Kaulimbiu ya mwaka huu ni Uandishi wa Habari na Changamoto za Kidijiti, ambayo inalenga kuangazia suala la uandishi wa habari na changamoto zinazoikumba sekta hiyo kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia duniani.
Post a Comment