Jana, Jumatatu, tarehe 16.5.2022, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) ilitoa MIKOPO ISIYOKUWA NA RIBA yenye thamani ya SHILINGI 198,799,602.
MIKOPO ilitolewa kwenye VIKUNDI 23 ambapo VIKUNDI 19 ni vya WANAWAKE, 3 vya VIJANA na 1 cha WATU WENYE ULEMAVU. Mgeni Rasmi alikuwa Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo
Mbunge huyo ameamua kugawa PLAU (jembe la kukokotwa na ng'ombe) moja kwa kila Kikundi kilichopata mkopo na kinachojishughulisha na KILIMO.
Mkurugenzi Mtendaji mpya, Ndugu Msongela Nitu Palela na Ofisi ya Maendeleo ya Jamii ya Halmashauri yetu, chini ya uongozi wa Ndugu Tana Ali Nyabange wanapongezwa sana kwa kazi nzuri.
Wanavijiji wa Jimboni mwetu wanakumbushwa yafuatano:
Wapeleke watoto wao wa chini ya MIAKA MITANO (5) wakapate CHANJO YA POLIO itakayofanyika Jimboni mwetu kati ya tarehe 18.5.2022 (kesho) na 21.5.2022. Chanjo zipo kwenye Zahanati na Vituo vyetu vya Afya.
Vilevile, WATAALAMU wetu wa AFYA wataenda nyumba kwa nyumba kutoa CHANJO ya POLIO kwa watoto chini ya miaka mitano.
Sensa ya Watu na Makazi itafanyika tarehe 23.8.2022. Wote tunapaswa kushiriki kikamilifu
Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO inayohusu MIKOPO iliyotolewa jana Jimboni mwetu.
Post a Comment