"Kwa hiyo vifaa vyote vipo na una uhakika wa kumaliza ujenzi ndani ya miezi miwili na nusu, kulingana na mkataba?" Ngalawa akamuuliza akamuuliza Mjezi wa nyumba hiyo Juma Masanja (kushoto) wa Kampuni ya Ujenzi ya ATIPA, alipofika eneo la ujenzi wa nyumba hiyo. Juma akajibu "Ndiyo Mkuu kila kitu kipo sawa".
Katibu Ngalawa akikagua mabati yatakayotumika kujenga banda la kuhifadhia baadhi ya vifaa vya ujenzi wa nyumba hiyo. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dar es Salaam, Mama Kate Kamba na wengine wanaoshuhudia ni Maofisa waandamizi wa CCM mkoa huo.
"Mwenyekiti, unaona kulee ndiyo mwisho wa eneo letu hili", akasema Ngalawa kumwambia Mama Kate Kamba.
Ngalawa akimuongoza Mama Kate Kamba kuendelea kukagua hatua za awali za ujenzi wa nyumba hiyo.
Ngalawa na Mama Kate Kamba wakitazama maandalizi ya ujenzi wa banda la kuhifadhia vifaa vya ujenzi wa nyumba hiyo.
Iddi Mvano kutoka Idara ya Uhasibu Ofisi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam, ambaye alitangulia kufika ene la tukio akimueleza jambo Mama Kate Kamba.
Uongozi wa CCM Wilaya ya Kigamboni chini ya Katibu mpya wa CCM wilaya hiyo Stanley Mkandawile ukiwa mstari wa mbele kusimamia ujenzi wa nyumba hiyo👇
"Sasa Wana CCM wenzangu eneo lenyewe la ujenzi wa nyumba ya Katibu wa CCM mkoa wetu wa Dar es Salaam, ndiyo hili, haya tungie kwa nguvu moja tuanze kuchapa kazi ya kusafisha kiwanja na kazi zingine", akisema Mkandawile baada ya yeye na viongozi wenzake wa wilaya hiyo na Vijana wa hamasa wa CCM kutoka UVCCM Kigamboni kuwasili kwenye eneo la ujenzi wa nyumba hiyo. Mwenye fulana la njano ni Katibu Mwenezi wa CCM wilaya hiyo Abdallah Pazi."Hizi kamba bila shaka ndiyo alama itakayowangoza mafundi wakati wa uchimbaji msingi", Katibu Mwenezi wa Wilaya ya Kigamboni Abdalaah Pazi akasema kuwaonyesha baadhi ya Viongozi wenzake wakiongozwa na Mkandawile (kulia)."Ngoja nisaidie kidogo hapa", Mkandawile akasema wakati akiweka sawa kigingi cha kama ya kuwekea alama ya uchimbaji msingi. Kushoto ni Mwenyekiti UVCCM Kigamboni.
Kisha Mkandawile akashiriki kukata mbao za kuandaa ramani ya uchimbaji msingi.
Mkandawile na Viongozi wenzake wakipalia nyasi kusafisha eneo la ujenzi. Kulia ni Pazi na kushoto ni Katibu wa UVCC Kigamboni Ndugu Kizigo
Mkandawile akishiriki kutoboa pipa la kutengenezea choo cha muda.
Iddi Mvano naye akashiriki kutoboa pipa hilo.
Mkandawile na Mvano wakiondoa udongo katika shimo lililochimbwa kwa ajili ya choo cha muda kwenye ujenzi wa nyumba hiyo.
Kijana wa hamasa akishiriki kusafisha eneo la ujenzi.
Vijana wa hamasa wa UVCCM wakishiriki kusafisha eneo la ujenzi huo.
Vijana wa hamasa wa UVCCM wakishiriki kusafisha eneo la ujenzi huo. |
Ukawadia wakati wa kupoza njaa baada ya kazi👇
Vijana wa Hamasa wa UVCCM wakiandaa mlo kwa ajili ya kupooza njaa wao na wenzao. Maandalizi ya kupatikana mlo huo yalifanywa na Katibu mpya wa CCM wilaya ya Kigamboni Ndugu Mkandawilie kwa kununua nyama na unga wa ugali.
Naam, nyama imeiva👍,"akasema Katibu wa UVCCM Ndugu Kizigo wakati akiionja nyama jikoni😀 |
Mlo ukaanza kupakulia tayari kwa kuliwa 'kijeshi jeshi'.
Mkandawile (kulia) akishiriki mlo huo pamoja na Vijana wa hamasa wa UVCCM. |
Mwenezi Pazi akishiriki chakula na Vijana wa kazi |
Mlo ukaendelea kuliwa.
Mlo ukaendelea kuliwa.
Mlo ukiendelea kuliwa.
Mlo ukiendelea kuliwa. Ni mikono ikikutana kwenye sahani.
"Nadhani kwa nafasi yetu kwa leo tumejitahidi kufanya kazi ya maandalizi ya ujezi wa nyumba ya Katibu wetu wa CCM wa mkoa wetu. Sasa mimi natangulia kuondoka kwenda kwenye majukumu mengine, mambo yote ya hapa nimeshaweka sawa", akasema Mkandawile wakati akiagana na Mvano kabla ya kuondoka. Mvano alibaki eneo la tukio kuwasubiri Mama Kate Kamba na Ngalawa.
© May 2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo
Post a Comment