Featured

    Featured Posts

WANAWAKE MTWARA WAKOSHWA NA RAIS SAMIA NA KUMPA TUZO MAALUM, SHAKA AIPOKEA NA KUSEMA NENO

Mtwara Vijijini
Mtwara Wanawake mkoani Mtwara, wamemkabidhi tuzo maalum Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idaya ya Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka kwenda kwa Rais Samia Suluhu Hassan kutambua mchango wake katika kuwatumikia Watanzania na kuwaletea maendeleo hususan mkoani humo.

Akipokea tuzo hiyo, Shaka, amesema tuzo hiyo itamtia moyo na kumpa ari Rais Samia katika kuwatumikia Watanzania.

"Kitendo cha kumpatia tuzo mnamtia moyo, mnapa ari ya kuwatumikia Watanzania, lakini pia mnamtia ari ya kutimiza malengo yenu akinamama katika mambo muhimu na ya msingi kama ambavyo nimeshasema.

"Mwito wangu kwenu msisite, msiishie hapa endeleeni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu, kila mmoja kwa imani yake Mwenyezi Mungu azidi kumpa afya njema ili aweze kututumikia Watanzania," amesema.

Akiendelea kuzungumza zaidi kuhusu tuzo hiyo, Shaka amesema aliyoyafanya Rais Samia wanawake wanayajua hata ukiwaamsha usingizini wanakwambia ameifungua Mtwara.

Awali akizungumza kabla ya kukabidhi tuzo hiyo, kwa niaba ya wanawake hao Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania Mkoa wa Mtwara, Zuhura Farid, amesema wanawake wa Mtwara kwa niaba ya wanawake wengine wote wanampongeza Rais Samia kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya.

"Hivyo tunaomba tukukabidhi zawadi hii kwa heshima na taadhima tunaomba umfikishie zawadi hii mama na umwambie asichelewe kufika Mtwara aje atuone kinamamma," amesema.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, akifurahi na baadhi ya Kinamamma, baada ya kuipokea Tuzo maalumu iliyotolewa na Wanawake wa mkoa wa Mtwara kwa Rais Samia Suluhu Hassan kutambua kazi nzuri ya kuwaletea maendeleo Watanzani hususan mkoa huo wa Mtwara, jana.

Wakati huohuo, Shaka, ameonyesha kukerwa na danadana zinazoendelea katika kupata utatuzi wa mgogoro wa ardhi kati ya wakazi wa eneo la kiwanja cha ndege mkoani Mtwara na mamlaka ya viwanja vya ndege.

Akizungumza alipotembelea eneo hilo kufuatilia maelekezo aliyoyatoa alipotembelea eneo hilo mwaka 2021, Shaka amesema danadana hizo hazina tija kwa wananchi na kutoa maelekezo kwa wizara nne kukutana haraka ili kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo.

"Ndugu zangu mimi nilisema nije na kuja kwangu ni kuweka msisitizo kwamba Chama kinafuatilia kwa karibu sana mgogoro huu, baina ya wananchi na mamlaka ya viwanja vya ndege na mamlaka zingine ambazo zimeingia katika kadhia hii.

"Kama kuna upande una haki, kama kuna upande hauna haki lakini unahitaji huruma basi mamlaka zinazokaa zikae zipime zitafakari uzito wa kuusaidia huo upande na athari endapo watausaidia huo upande ni zipi na mwisho waje na majibu ili wananchi hawa waishib kwa amani, ili wananchi hawa waishi kwa utulivu.

"Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ipo pamoja na ninyi, na ipo pamoja na ninyi katika kuhakikisha mgogoro huu unafikia mwisho," amesema.

Ameema wizara nne zinahusika katika utatuzi wa mgogoro huo, hivyo ameziagiza kukutana haraka iwezekanavyo ili kuutafutia ufumbuzi na kwamba kama zimeshindwa kutatua basi waeleze ili suala hilo lipelekwe katika ngazi za juu zaidi.

"Ukifuatilizia hapa kuna karibu wizara tatu zinaingia kwa nne. Wizara ya Uchukuzi ambao ndio wana mamlaka ya viwanja vya ndege, wizara ya Nishati ambao wao wana dhamana ya gesi, wizara ya tamisemi ambao wao wana watu na wizara ya ardhi ambao wamepewa mamlaka ya kisheria kusimamia mambo ya ardhi.

Sasa taasisi moja inapokuwa mlalamikaji kwamba wenzake hawapo tayari kutoa ushirikiano ni jambo linalosikitisha sana ndugu zangu huko serikaliini.

"Maelekezo ya Chama ni kwamba, taasisi hizo nne nilizozitaja zikutane haraka sana kujadili kadhia hii na waje na majibu ya kuwapa wananchi hawa," ameagiza.

Shaka ametoa agizo hilo baada ya Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Mkoa wa Mtwara, Samuel Miruma kusema kusuasua kwa utatuzi wa mgogoro huo kunachangiwa na baadhi ya taasisi zinazohusika kuchelwa kutoa ushirikiano.

Wakazi wa eneo la Kiwanja Cha Ndege Wakiwa wakimunesha jumbe mbalimbali  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, kuomba utatuzi wa mgogoro wa ardhi kati ya wakazi hao wa eneo la Kiwanja cha Ndege wenye mgogoro na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege mkoani Mtwara, jana.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana