Askofu, Dkt Evance Chande wa Kanisa la Karmel Assemblis of God, amenukuu kwenye Biblia jinsi Mungu alivyohimiza kujua hesabu za watu, hivyo kuwataka watanzania wote kuungana na Rais Samia Suluhu Hassan kuhamasisha watu kujitokeza kwa wingi siku ya Sensa Agosti 23, 2022.
Chande ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Mkoa wa Dodoma, ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanahabari katika mkutano na viongozi wa dini pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu anayewakilisha wafanyakazi, Dkt Alice Kaijage jijini Dodoma Agosti 15, 2022.Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Askofu Dkt Chande pamoja na mambo mengine akinukuu kwenye Biblia neno la Mungu kuhusu sensa....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
Post a Comment