Uvinza, Kigoma
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara Christina Mndeme amewaagiza Tanesco kufunga mara moja Transfoma ya umeme ndani ya siku tano ili kuwezesha mtambo wa maji kuanza kufanya kazi katika Kijiji cha Mlela, Kata ya Kandaga mkoani Kigoma.
Mndeme ametoa agizo hilo Agosti 6, 2022 baada ya kukagua ujenzi wa tenki la maji katika Kijiji hicho cha Mlela Wilayani Uvinza akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Kigoma, na kubaini kwamba licha ya mradi kukamilika lakini wananchi hawapati maji kutokana na kutokuwepo kwa muda mrefu Transfoma ya umeme kwenye mtambo wa kusukuma maji.
"Haiwezekani na haiingii akilini wananchi mnakosa maji tangu mwezi wa saba hadi leo kwa sababu tu ya umeme kutofika kwenye pampu, haiingii akilini, maji hayana mbadala." alisema Mndeme", akasema Mndeme.
Tafadhali, Msikilize Mndeme, Hapo👇
Post a Comment