Featured

    Featured Posts

SHAKA: HATUA YA RAIS SAMIA KUONGEZA BAJETI YA KILIMO KUTOKA SH. BILIONI 254 HADI SH. BILIONI 954 ITALETA MABADILIKO MAKUBWA KIUCHIMI

Na Mwandishi Maalum, Morogoro
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan, kuitazama kwa karibu sekta ya kilimo, ikiwemo kuongeza bajeti ya Wizara Kilimo, kutoka sh. Bilioni 254 mwaka wa fedha 2021/2022 hadi Sh. bilioni 954 sawa na asilimia 224 kwa 2022/2023, italeta mabadiliko makubwa katika uchumi.

Akizungumza jana, alipotembelea Maonyesho ya Kilimo ya Nanenane Kanda ya Mashariki, mkoani Morogoro Shaka amesema, miongoni mwa mabadiliko hayo katika Uchumi ni pamoja na kuwezesha kutengenezwa fursa nyingi za ajira akifafanua kuwa hadi kufikia mwaka 2025 vijana na wanawake zaidi ya milioni 3 watanufaika na ajira hizo.

Shaka amesema, maelekezo ya  Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 - 2025, katika Ibara ya 8 kifungu f  imeahidi katika kipindi cha miaka mitano zitazalishwa ajira milioni 8 kwa Watanzania, sasa kwenye kutafsiri maelekezo ya Ilani hiyo Serikali ya Awamu ya 6 chini ya Rais Samia imeshajiwekea mwelekeo au matatarajio yake katika ajira hizo kupitia sekta ya kilimo.

Tafadhali, Msikilize Shaka, Hapo👇

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana