Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa DAWASA imedhamiria mwaka 2023 kumaliza kabisa kero ya maji katika jiji hilo kwa asilimia 100 na kwamba hivi sasa wamefikia asilimia 96 utoaji wa huduma hiyo. Luhemeja ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika Idara ya Habari-MAELEZO jijini Dodoma Agosti 13, 2022, kuelezea utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji katika Jiji hilo na maeneo ya jirani.
Baadhi ya wanahabari, Afisa wa DAWASA na MAELEZO wakiwa katika mkutano huo.
PICHA NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Mhandisi Luhemeja akielezea mafanikio hayo....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203
Post a Comment