Featured

    Featured Posts

KINANA APIGA KURA KUCHAGUA VIONGOZI WA CCM OYSTERBAY

 Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, ameshiriki pamoja na wana CCM wa Kata ya Oysterbay kuwachagua viongozi wapya wa Chama katika kata hiyo.

Uchaguzi huo umefanyika Agosti 6, 2022 katika Shule ya Msingi Oysterbay jijini Dar es Salaam ambapo viongozi mbalimbali wamechaguliwa.

Akiwasalimia wana CCM wenzake baada ya upigaji kura, Kinana amesema Chama kinafurahishwa na mwitikio mkubwa wa wanachama kujitokeza kuomba nafasi mbalimbali na kufanya uchaguzi kwa amani.

Kinana amesema hadi sasa mwenendo wa uchaguzi unakwenda vizuri na kwamba changamoto chache zinazojitokeza hususani kuhusu  malalamiko ya ukiukwaji wa haki, hatua zitachukuliwa na haki itatendeka.

“Yapo malalamiko ya hapa na pale, lakini nina hakika yatafanyiwa kazi ili mwanachama akishinda ashinde kwa haki.
Msingi wa Chama hiki ni kutenda haki, kwa hiyo nina hakika viongozi watatenda haki,” amesema Kinana.

Nafasi zilizopigiwa kura ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Oysterbay, wajumbe wa mkutano mkuu wa mkoa,wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya na wajumbe wa halmashauri kuu ya kata hiyo

 

 

 

 

 

 

 

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana