Kasi ya kusambaza maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria inaongezeka siku hadi siku ndani ya Jimbo letu - Ahsante sana Serikali yetu chini ya uongozi mzuri sana wa Rais wetu, Mh SAMIA SULUHU HASSAN.
Vijiji vya Kata ya Nyambono na Kata ya Bugoji vimeanza kupata maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria.
Vijiji hivyo ni:
Kata ya Nyambono
Kijiji cha Nyambono
Kijiji cha Saragara
Maji haya ya bomba yatapelekwa hadi Kijiji cha Mikuyu, Kata ya Nyamrandirira
Vijiji hivi vimejengewa TANKI la LITA 200,000 Mlimani Nyabherango (Bajeti ya Mwaka 2021/2022)
Kata ya Bugoji
Kijiji cha Bugoji
Kijiji cha Kanderema
Kijiji cha Kaburabura
Vijiji hivi vimejengewa TANKI la LITA 200,000 za maji Mlimani Nyabherango
Vyanzo vya FEDHA za Serikali za Mradi huu ni:
UVIKO- 19: Tshs 500m
EP4R: Tshs 480m
RUWASA inafanya kazi nzuri sana Jimboni mwetu - Hongereni sana!
Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO yenye shukrani za Wanavijiji wa Jimbo la Musoma Vijijini - imeambatanishwa hapa.
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo anaendelea kuhamasisha SENSA ya WATU na MAKAZI Jimboni mwetu. Leo atakuwa Kata za Ifulifu (Vijiji 3) na Nyakatende (Vijiji 4)
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
https://ift.tt/MRdvmW7

Post a Comment