Buchosa, Sengerema
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Tanzania Bara Christina Mndeme ameitaka Bohari ya Dawa (MSD) kuacha urasimu na kuiagiza kupeleka dawa haraka katika Kituo cha Afya cha Buchosa kilichopo Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza.
Pia, amemuagiza Mhandisi wa Halmashauri ya Buchosa kufuatilia kwa karibu zaidi mwenendo wa ujenzi wa Kituo hicho cha Afya cha Kuchosa.
Mndeme ametoa maagizo hayo jana, Agosti 10, 2022, alipotembelea na kukagua kituo hicho cha Afya, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza. Tafadhali Msikilize Hapo👇
Post a Comment