"Serikali ya CCM Awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan inawekeza fedha nyingi kwenye miradi ya ujenzi wa miundombinu kote nchini.
Chama kinashauri fursa za ajira zinazotokana na miradi hii zianze kuwanufaisha kwanza wananchi wa maeneo ambako miradi hiyo inatekelezwa au inapita wakiwemo vijana. Hivyo wakuu wa wilaya na mikoa wasimamie hili." Amesema Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka yupo mkoani Tabora kwa ziara ya siku tano 16-20 Agosti, 2022 akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya CCM Umoja wa Wazazi Tanzania Ndg Gilbert Kalima.
Post a Comment