Featured

    Featured Posts

MAKAMU WA RAIS DK. MPANGO AKUTANA NA IGP WAMBURA

Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango leo tarehe 18 Agosti 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali wa Polisi Camillus Wambura, Mazungumzo yaliofanyika ofisini kwa Makamu wa Rais Jijini Dar es salaam.

 

Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amelipongeza jeshi la polisi kwa kuendelea kuimarisha amani pamoja na ulinzi wa wananchi na mali zao. Amesema kazi ya kulinda Raia na mali zao ndio msingi wa maendeleo ya nchi hii hivyo jeshi la polisi linapaswa kuendelea kuhakikisha utulivu unapatikana wakati wote.

 

Aidha Makamu wa Rais amelitaka jeshi hilo kutenda haki pasipo kuonea mtu yeyote na yeyote anayevunja sheria achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria na sio vinginevyo. Makamu wa Rais amemuagiza IGP Wambura kuangazia malalamiko yanayotolewa na wananchi kwa jeshi la polisi na kuwachukulia hatua askari wachache wanaoharibu taswira ya jeshi hilo.

 

IGP Wambura amefika kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kujitambulisha mara baada ya kuteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Makamu wa Rais Dk. Mpango akozungumza na IGP Wambura
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana