Na Bashir Nkoromo, Kimara
Kikundi cha Youth For Impact Tanzania (YFIT) leo kimetoa msaada wa fedha taslimu na vitu vya mahitaji mbalimbali kwa wasichana zaidi ya 60 wenye shida na kusema hatua hiyo ni kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika juhudi zake anazofanya katika kuwakomboa Wanawake kutoka katika shida.
Wasichana hao wanaishi pamoja nyumbani kwa mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam Dk. Consoler Eliya kama familia ya mkazi huyo ambaye anasema aliwakusanya kwa nyakati tofauti wakiwa ni watoto wanaoishi katika mazingira magumu na anasema hapo nyumbani kwake na mumuwe siyo Kituo cha kulea watoto wenye shida.
Dk. Consoler anasema kuwa japokuwa wasichana hao aliwakusanya kwa nyakati tofauti wakiwa wanaishi katika mazingira magumu na kuwaweka nyumbani kwake kisha kuwatafutia huduma mbalimbali ikiwemo kusoma, hapendezwi kusema kwamba anawalea katika Kituo cha kulelea Watoto wenye shida kwa sababu kusema hivyo siyo sahihi.
"Unajua kila mtoto anapaswa kulelewa kifamilia, sasa unapomchukua na kusema unamlea katika Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu bado unamuathiri kisaikolojia, ndiyo maana Wasichana hawa, nawaita ni familia na kwa kweli wanajisikia wanaishi kifamilia, maana nawalea kifamilia", akasema Dk. Condoler ambaye ni Mama wa Watoto wawili na anaishi na mumuewe Eliya.
Dk. Consoler anasema, tangu aanze kukusanya wasichana wanaoishi katika mazingira magumu, watoto wameshafikia zaidi ya 100 na hadi sasa wapo waliokwishaolewa na wanaosoma hadi vyuo vikuu mbali na hao 60 alionao sasa ambao wamesoma tangu chekechea na wengine sasa wapo vyuo vikuu.
"Mimi nilijiwa na wazo kwamba kuna haja ya kuwa na 'Foundation' kwa ajili ya kusaidia kutatua au kupunguza changamoto ambazo huwakabili Wasichana, baada ya kuanzisha 'Foundation' hii ya YFIT nikawatafuta marafiki zangu tushirikiane, nikawapata wa Shule ya Laureate International School. Kwa hiyo leo tumeleta msaada wa vitu vingi kiasi ikiwemo vyakula, nguo, taulo za kike na fedha taslimu ili kuwasaidia wasichana hawa, tumejisikia fura sana", akasema Harriet Sigalla wakati akikabidhi msaada huo kwa niaba ya marafiki zake kadhaa aliokuwa nao katika hafla hiyo.
Harriet akasema " Hizi hatua hii ya kutoa misaada kama huu, pia ni kuunga mkono Rais wetu Samia Suluhu Hassan katika juhudi zake amnazofanya kila siku katika kumnasua mwanamke hasa mtoto wa kike kutoka katika mazingira magumu, kwa kweli ninampongeza na kumshukuru sana Rais Samia, maana jitihada zake katika hili na mengine zinaonekana".
Katika hafla hiyo Harriet aliambana na Mwanzilishi msaidizi wake wa YFIT Lorraine Lyimo, Mraribu wa kikundi hicho Ndabaningi Mwakalyelye, baadhi ya Wanafunzi na walimu kutoka Shule za Laureani International Schools, Mwenyekiti wa UWT Kata ya Saranga Rose Merere (Mama yake Harriet) na Katibu wake Levina Mlokozi.
Harriet ni Mwanzilishi wa YFIT ni mwanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Cambridge jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi wa Kikundi cha Youth For Impact Tanzania (YFIT) Harriet Sigalla akikabidhi msaada wa fedha taslim kwa Dk. Consoler Eliya (kushoto) alipofika nyumbani kwa Dk. Consoler yeye na rafiki zake kutoa msaada wa fedha na vifaa vya mahitaji mbalimbali kwa ajili ya Wasichana zaidi ya 60 wanaolelewa nyumbani kwa Dk. huyo, Kimara Jijini Dar es Salaam, leo.
Harriet akizungumza jambo na Dk. Consoler kabla ya shughuli kuanza rasmi. Katikati ni Mwanzilishi msaidizi wa YFIT Lorraine Lyimo.
Mwenyekiti wa UWT Kata ya Saranga Rose Merere (kulia) ambaye ni Mama yake Harriet akisalimiana na Dk. Consoler mwanzoni mwa hafla hiyo.
Harriet (Katikati) akishauriana jambo la Lorraine na Ndabaningi (kushoto) mwanzoni mwa hafla hiyo.
Mratibu wa YFIT Ndabaningi Mwakalyelye akimkaribisha Harriet kuzungumza kabla ya kukabidhi msaada.
Harriet akizungumza maneno muhimu kabla ya kukabidhi msaada. Kulia ni Katibu wa UWT Kata ya Saranga Levina Mlokozi ambaye alihudhuria hafla hiyo.
Mlezi wa Wasichana 'Wanafamilia' Dk. Consoler akizungumza kabla ya kukabidhiwa msaada.
Baadhi ya marafiki wa Harriet kutoka Shule ya Laureate International School (kushoto) wakimsikiliza Dk. Consoler.
Katibu wa UWT kata ya Saranga na baadhi ya waliohudhuria wakimsikiliza Dk. Consoler
Msichana mwanafamilia nyumbani kwa Dk. Consoler, Queen Omar, akizungumza naneo la shukurani na kufanya maombi ya shukurani.
Wasichana wanafamilia, wakipokea dua ya shukurani
Wahudhuriaji wakipokea maombi ya shukurani
Harriet akikabidhi wasichana wanafamilia taulo za kike.
Harriet na marafiki zake wakiendelea kukabidhi misaada ya vitu kem kem.
Harriet akimkadhi madaftari Dk. Consoler
Harriet akimkabidhi Dk. Consoler ndoo ya sabuni ya unga.
Baada ya kukabidhi ikawa shangwe.
Harriet akimkabidhi Dk. Consoler orodher ya vifaa alivyotoa
Mratibu wa YFIT Mwakalyelye akifunga shughuli
Harriet akikumbatiana na Dk. Consoler kwa furaha baada ya makabidhiano ya msaada.
Picha ya pamoja,
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja
"Ahaaa, kaeni vizuri, hii itakuwa picha ya mwaka😀" akasema Harriet wakati akiwapiga picha Dk. Consoler na wageni waliofika kwenye hafla hiyo.
Wasichana wanafamilia ya Dk. Consoler wakibeba zawadi kwenda kizihifadhi. ©August 2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo
Post a Comment