Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akimvisha kanga ya Nyamitwe Maganga mkazi wa Ushokola katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Tabora. (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).
Shaka akisikiliza kero kutoka kwa Nyandwi Dubo (aliyeshika vipazasauti) huku wananchi wakifuatilia mkutano katika Kijiji cha Ushokola katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Tabora.
Shaka akicheza Ngoma yenye asili ya Wanyamwezi katika Kijiji cha Ushokola, Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, mkoani Tabora akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Tabora.
Shaka akishiriki ujenzi wa kituo cha Afya Ifuta kilichopo katika Kata ya Ukondamoyo, Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, mkoani Tabora akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Tabora.
Shaka akiwa ameungana na wananchi waliohudhuria shughuli ya ujenzi wa kituo cha Afya Ifuta, Kata ya Ukondamoyo, Wilaya ya Urambo mkoani Tabora wakicheza nyimbo za asili, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Tabora.
Mbunge wa Urambo Mashariki mkoani Tabora, Margaret Sita, katika ujenzi wa kituo cha Afya Ifuta kilichopo katika Kata ya Ukondamoyo Wilaya ya Urambo mkoani humo ikiwa sehemu ya ziara ya Shaka kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Na MWANDISHI WETU, TABORA
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa(NEC) ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ameziagiza halmashauri zote nchini kuwasimamia wakandarasi wanaowapa nafasi za kutoa huduma ili kulinda haki za wananchi ambao wengi wao wamekuwa wakilalamika kudhulumiwa.
Akizungumza jana mbele ya wananchi wa Kijiji cha Ushokola wilayani Kaliua mkoani Tabora Shaka alisema kumekuwa na utaratibu wa kuwapangia wakandarasi kandarasi za mirdi katika maeneo mbalimbali lakini wapo baadhi wanapomaliza kazi hawataki kulipa haki za watu.
“Sio sahihi , niwaombe sana halmashauri zote nchini kuwasimamia wakandarasi wanaowapa nafasi za kutoa huduma iwe kandarasi ya ujenzi wa barabara , iwe kandarasi ya ujezi wa vituo vya afya.
“Iwe kandarasi za kutoa huduma katika halmashauri tuwaombe sana wakati wanapoharibu kazi jambo la kwanza simamieni haki za wanyonge waweze kuzipata.Haiwezekani mkandarasi anapewa kazi analipwa fedha na halmashauri.
“Lakini anaharibu kazi anaondoka, anaacha mzigo wa madeni ya wananchi wanyonge sio sahihi kabisa kabisa jambo hili na wala sio ubinadamu.Niwaombe sana na niwasihi ndugu zetu mliopewa dhmana katika halmashauri mkiwemo wakuu wa wilaya simamieni hili kuhakikisha mkanndarasi anapoharibu kazi au kumaliza mkataba wake jambo la kwanza angalieni hana madeni ya wananchi wa chini, “alisema Shaka.
Aliongeza jambo la la msingi wajiridhishe hakuna haki za watu ambazo zinakwenda kupotea kwa wale waliokuwa wakitoa huduma wakiwemo vibarua waliokuwa wakiwafanyisha kazi.“Tukilifanya hili tutakuwa tumejenga uimara lakini tutakuwa tumeondoa na kutokudumaza hali za wananchi wetu.”
Shaka aliamua kutoa maelekezo hayo kwa halmashauri baada ya kupokea kilio cha mmoja wa wananchi wa Kaliua ambaye alidai kuna mkandarasi amemfanyia kazi kwa miaka mitatu lakini alipoondoka hajamlipa haki zake.
“Huyu mama inasikitisha hali yake hii na ametoa huduma kwa zaidi ya miaka mitatu mkandarasi ameshindwa kazi , mkandarasi anaondoka anaacha mzigo wa madeni , huyu mama na yeya mpaka anatoa huduma alijitengeneza , alijiunga jiunga mpaka akapata nguvu ya kwenda kumhudumia huyo mkandarasi
“Kumuacha na mzigo wa madeni sio sahihi kabisa, kwa hiyo kupitia kwa mama huyu kwasababu kila tunapokwenda imekuwa ndio kilio watu wanaporibu kazi wanaacha mzigo wa madeni halafu hawa wengine wanahangaika huku chini jambo hili niombe sana mlimchukue na likafanyiwe kazi,”alisema Shaka.
UJENZI MIUNDOMBINU YA BARABARA
Katika hatua nyingine Shaka alitumia nafasi hiyo kuelezea hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo ya wananchi wakiwemo wa Wilaya ya Kaliua, Mkoa wa Tabora na nchi kwa ujumla .
“Nataka kuchukua nafasi hii kumpongeza kwa dhati kabisa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo watanzania , mmenituma nije nikague barabara hii ambayo inajengwa kwa kilometa 2.7 hapa Kaliua lakini kwenye Wilaya hii Rais Samia ndani ya kipindi kifupi sana cha uongozi wake anakwenda kujenga barabara kilometa 10.
“Jambo ambalo halijawahi kutokea tangu nchi imepata uhuru na kwa mara ya kwanza kabisa ndani ya Wilaya hii Rais Samia ndio anajenga barabara za lami. Anawajengea barabara lakini wakati huo huo anawawekea na taa inamaana Kaliua inakwenda kuwa ya kileo.
“Kwa hiyo wote kwa pamoja tumpongeze Rais Samia ,wote tumekuwa mashuhuda namna ambavyo Rais Samia amesimama kidete kufungua uchumi wa mtu mmoja mmoja lakini uchumi wa kikanda na uchumi wa kimaeneo.Kukamilika kwa barabara hizi kilometa 10 ni hatua mpya ya kufungua uchumi wa wana Kaliua.
“Mtasafirisha mazao lakini mtarahisisha maisha yenu ya kila siku kwa kuhakikisha kuwa huduma za kijamii zinapatikana kwa urahisi zaidi.Kazi hii sio kazi ndogo kumpata Rais mwenye maarifa , mwenye mawazo lakini kupata Rais ambaye anafikiria wananchi wake wanahitajia nini na kwa wakati gani,”alisema Shaka.
Aliongeza ni jambo la kumshukuru Mungu, tunaye Rais anayejua wananchi wake wanataka nini , lakini tunaye Rais ambaye kwa wakati huu anajua wana Tabora wanahitaji nini.
“Lakini tunaye Rais ambaye anajua wana Kaliua wanataka nini , hasa kuliona hilo kwa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan nadhani wote mmesikia amesaini mikataba 10 kwa niaba ya mikataba 968 ambayo inakwenda kujenga barabara za kisasa kabisa.
“Anakwenda kufungua miundombinu ya barabara nchi nzima, mikataba hiyo fedha ni nyingi mno zinazokwenda kutumika zaidi ya Sh.bilioni 248 kwa ajili ya kujenga miundombinu ya barabara ndani ya nchi yetu.Niwaombe wananchi itakapokamilika barabara hizo tutunze ili ziishi kwa muda mrefu,”alisema Shaka.
Aidha aliwaomba wananchi wote kuendelea kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan kwa nia njema aliyokuwa nayo akitoa mfano kwamba Kaliua wameanza kuona maajabu.“Kaliua mlitegemea kuyaona haya nani kama Rais Samia, kwa hiyo maendeleo haya naomba myathamini sana.”
Post a Comment