Featured

    Featured Posts

TANI 21 ZA KAHAWA MAGARI 4 PIKIPIKI NA BAISKELI KADHAA VYAKAMATWA KATIKA ZOEZI LA KUTHIBITI MAGENDO YA KAHAWA WILAYANI KYERWA.

Mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Bwana Musa Jumanne akizungumza katika Kikao hicho
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa Bahati Henerico akitoa taarifa ya maendeleo ya wilaya hiyo


Na Lydia Lugakila

Kyerwa'

Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera kupitia kikosi maalum cha kudhibiti magendo

imefanikiwa kukamata tani 21 za kahawa magari 4 pikipiki na baiskeli kadhaa katika zoezi la kudhibiti magendo ya kahawa.

Akizungumzia tukio hilo kupitia kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bahati Henerico amesema vifaa hivyo vimekamatwa wakati wa zoezi la udhibiti wa magendo ambapo wamefanikiwa kukamata kahawa iliyokuwa katika harakati za kutoroshwa kwenda nje ya nchi pamoja na kumilikiwa kinyume na sheria katika mazingira mbali mbali. 

Kufuatia hali hiyo mwenyekiti huyo amemuomba mgeni rasmi katika kikao hicho Bwn,Musa Jumanne kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo kutoa maelekezo ya serikali kwa wananchi ambao dira ya siyo ya kuuza kahawa hapa nchini bali mpango wao ni kuipeleka nje ya nchi.

Aidha kupitia kikao hicho Bwn Jumanne amewaomba wananchi wa wilaya hiyo walio na kahawa kuweka njia nzuri kuipeleka katika vyama vya msingi AMCOS huku akiahidi kuanza kwa msako mkali wa kujua ni akina nani wana kahawa ili sheria ichukukue mkondo wake.

"Kikosi cha kudhibiti magendo kinaendelea kupambana na wale wanaomiliki kahawa majumbani na wale wanaowaza kuivusha kahawa nje ya nchi tutawakamata alisema Jumanne.

Naye mbunge wa jimbo la Kyerwa innocent Bilakwate amesema kuwa wananchi wanatakiwa kutambua ili serikali iwaunge mkono katika shughuli za maendeleo mapato yanayopatikana ndiyo yanayosaidia miradi mbali mbali kwa wananchi.

Bilakwate amempongeza  Rais Samia kwa kuhakikisha anaweka utaratibu mzuri wa kahawa kuuzwa kwa njia nzuri ambapo utaratibu huo  umesaidia wakulima walionyonywa kunufaika na zao hilo.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana